Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
Wananchi mbalimbali wanaotaka katiba mpya wameshtushwa na ubaridi wa ghafla wa chama cha Demokrasia na maendeleo (ChADEMA) katika kudai katiba mpya.
Watu hao wanasema walikuwa na tumaini kubwa sana kuwa kupitia pressure ya taasisi hiyo yenye nguvu nchini pamoja na kuunganisha nguvu za wananchi wengine wanaotaka katiba mpya basi ingeweza kupelekea katiba hiyo kupatikana.
Kabla ya Mwenyekiti Mbowe hajaenda jela na wakati akiwa jela vuguvugu la chama hicho kudai katiba mpya lilikuwa kubwa sana hadi kufikia watu kudhani kuwa Mbowe alikamatwa na kuwekwa ndani sababu ya Kudai katiba mpya!
Cha ajabu baada ya Mbowe kutoka jela amekuwa hana tena msisitizo wa kuzungumzia katiba mpya, hata anapopata nafasi ya kuongea ni kama anakwepakwepa kuzungumzia katiba mpya.
Siku hizi hata maoamanda wao akina Lema, Lissu na vijana wa Chadema wamepunguza kasi ya kudai katiba mpya siyo kama mwanzo.
Watu sasa hivi mitandaoni wanahoji, je CHADEMA imeshabadili gia angani kama kawaida yake?, Wengine wanahoji kuwa au tayari Jamaa wameshavuta mpunga ndiyo maana wameanza kupunguza pressure ya kudai katiba mpya?.
Watu wanahoji haya hasa ukizingatia historia ya viongozi na watu waandamizi wa CHADEMA huko nyuma "kuunga mkono juhudi" na kwenda CCM kitu ambacho ni dhahiri ni kununuliwa.
Hapa chini ni sauti ya Mwananchi huko clubhouse ikihoji kupoa huko kwa Chadema kudai katiba mpya wakati tayari ilishakuwa ni ajenda kubwa na wananchi wameipokea.