Watu wakubwa baada ya gharika

Watu wakubwa baada ya gharika

Jackwillpower

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2017
Posts
2,467
Reaction score
3,687
Leo tutawatazama vizazi vya watu wakubwa katika historia ya Biblia baada ya gharika, kwa mujibu wa Biblia kulikuwa na vizazi vya watu wakubwa sana, mfano kama ilivyo leo katika jamii tofauti ama maeneo fulani kuna watu wakubwa kama Hashim Thabiti ambaye ana futi 7.2. Lakini katika zama za Biblia walikuwa wakubwa zaidi kulinganisha na leo.

Jamii hii ya watu wakubwa ilipatikana katika nchi ya Kanaan, nchi ambayo ilikuwa tajiri sana kwa chakula na uoto wa asili na miti mikubwa ya Mierezi ya Lebanon. Nchi hii ilikaliwa na wana wa Hamu hasa Kanaani. Vizazi hivi vya watu wakubwa bilashaka walikuwa uzao mmoja uliogawanyika katika koo, kama koo ya Warefai, Wazuzi, Waemi na Waanaki. Jamii hii ilikuwa na vizazi vya kutisha ambavyo viliogopeka. Lakini cha ajabu vizazi hivi vya watu wakubwa viliangamizwa na wazao wa Yakobo [Israeli], Esau [Edom] na Lutu [Moabu na Amon] ambao wote wana asili ya mzee Ibrahimu baba wa Imani. Na hivyo vizazi vya majitu ni kama ifuatavyo.

FB_IMG_1650478599927.jpg

KIZAZI CHA REFAI

Warefai maana yake ni watu wakubwa au watu wa kuogopesha, Biblia ya KJV imetafsiri Warefai kuwa GIANTS. Hawa walikuwa watu wenye nguvu na wengi, warefu kama Waanaki wameanza kuonekana katika enzi ya Ibrahimu. Waamoni waliwaita Wazamzuni kulingana ujamii wao na Wazuzi. Warefai waliishi mashariki ya mto Yordani. Walishambuliwa na muungano wa majeshi yaliyoongozwa na mfalme Kedorlaoma mfalme wa Elam/Iran. [Mwanzo 15:5, ]. Hivyo Kanaani ikawekwa chini ya mfalme huyu, lakini mda punde Kanaan ikakombolewa na mzee Ibrahimu aliyemshinda mfalme huyo wa Iran na kumnyang’anya mateka na nyara zote alizozitwaa huko Kanaan pamoja na kumwokoa Lutu mpwa wake, aliyekuwa mmoja wa mateka hao. Hivyo Warefai waliendelea kuishi mashariki mwa Kanaani mpaka walivyokuja kuangamizwa na wana wa Amoni [mzao wa Lutu] waliomiliki eneo hilo baada yao. [Kumb 2:20,21].

Eneo hili sasa ni nchi ya Jordan. Warefai baada ya kuangamizwa na wana wa Amoni, walibakia masalia, mmoja wao ni Ogu ambaye aliishi Bashani [sasa ni Syria] na kuwa mfalme huko. Ogu alikuwa mkubwa sana mwenye urefu wa futi 13, kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa futi 13.5 na upana wa futi 6, hivyo alikuwa mrefu zaidi ya Goliath mwenye futi 9. [Kumb 3:11]. Jeshi la Israeli likiongozwa na nabii Musa lilimwangamiza Ogu na jeshi lake lote la Waamori, ilikuwa ni baada ya Ogu kuwavamia Waisraeli walipokuwa wanatoka Misri. Nchi ya Ogu na miji yake 60 Musa aliitwaa na kuwapa wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, na hiyo nusu ya kabila ya Manase, mwana wa Yusufu. [Hes 32:33].

KIZAZI CHA ZUZI

Kizazi cha Wazuzi ndio hao Wazamzumi. Nao ni watu wakubwa, warefu, kama Waanaki [Kumb 2:20].” Kinachojulikana pia ni kwamba Wazamzumi waliishi katika mji wa Hamu [Mw 14:5], wakipewa dalili zaidi ya ukoo wao kupitia Hamu na haswa mwanawe Kanaani (ambaye uzao wake ulitawala sana Nchi ya Ahadi na eneo lote lilipewa jina lake). Wachambuzi wengine wa Biblia na wasomi wanafundisha kwamba baada ya gharika Hamu aliondoka mashariki na kuhamia eneo ambalo leo linajulikana kama Afrika, Biblia inathibitisha kwamba wazao wa Hamu kwa sehemu kubwa waliishi katika eneo ambalo leo ni Mashariki ya Kati.

Katika Mwanzo 14:5 tunaona pia Wazuzi wanapitia zahama kama waliyopitia Warefai na Waemi kutoka kwa uvamizi wa Kedorlaoma. Hivyo jamii hii ya watu wakubwa imetokana na mtu mmoja ambaye ni Hamu ingawa waliishi kikoo na mda mwingine walichanganywa kwa majina yao kwasababu walionekana katika ufanano wa ukubwa. Hamu ndiye baba wa Wakushi pia ambao pia wanajulikana kwa urefu wao na ushujaa. Biblia inawasema hivi, “watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu,wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao. [Isaya 18:2].” Kizazi cha Wakushi mpaka sasa kina watu warefu na laini ingawa nchi yao imeenea vita sasa. Wazuzi katika Hamu pamoja na Warefai ndugu zao, walikuja kuangamizwa na watoto wa Lutu kwa msaada wa Mungu, na nchi yao ikamilikiwa na watoto wa Lutu.

KIZAZI CHA EMI

Waemi kwa mujibu wa Biblia walikuwa watu wakubwa mno [giants] na warefu sawa na ndugu zao hao Warefai, wameanza kusemwa katika kitabu cha Mwanzo 14:5. Walikuwa ni watu wa vita lakini pia walishindwa na mfalme Kedorlaoma na washirika wake katika uwanda wa Kiriathaim. Nao walikaa mashariki mwa mto Jordan katika zama za Ibrahimu. Waemi pia walidhaniwa kuwa Waanaki, huenda sababu ya urefu na ukubwa wao sawa na Waanaki, lakini Wamaobi waliwaita Waemi. Waliangamizwa na jeshi la Wamoabu (uzao wa Lutu) na kunyang’anywa nchi yao. [Kumb 2:10-11].

FB_IMG_1650478608890.jpg


KIZAZI CHA ANAKI

Anaki alikuwa ni mtoto wa Arba, Arba alikuwa ni jitu kubwa sana [giant] kuliko wote, ambaye pamoja na uzao wake [Waanaki] waliishi kusini mwa nchi ya Kanaan. Alijenga mji na kuuita kwa jina lake yaani Kiariath Arba [mji wa Arba], mji huu baadae uliitwa Hebron. [Yoshua 14:15]. Hebron ndio eneo ambalo wazee wa Imani na wake zao walizikwa (Ibrahim, Isaka na Yakobo). Wakati mwingine nitauzungumzia mji huu. Hivyo Arba ndio baba wa Anaki na Anaki ndio baba ya Waanaki ambao walikuwa wakubwa lakini si kama Arba babu yao. Muonekano wao ulikuwa ni wakutisha, kama ilivyoelezewa na wapelelezi Kumi na Wawili waliotumwa kuipeleleza nchi ya Kanaani, walirudi na habari mbaya iliyowajaza Waisraeli hofu. Wapelelezi walidai wamewaona wana wa Anaki, watu watatu wakubwa warefu na kuwahusisha na Wanefili, (wa zama kabla ya gharika), na kudai kwamba walijiona kama Panzi mbele yao. (Mwanzo 6:4, Hesabu 13:33). Hivyo walipandikiza hofu ambayo ilisababisha uasi wa kitaifa, taifa zima likamwasi Musa na Mungu na kusababisha adhabu ya kuzunguka jangwani kwa miaka 40, ili kizazi cha uasi kipuputike kasoro Yoshua na Kalebu. [Taz Hesabu 14]. Kwa mujibu wa nabii Musa, aliwasema hivi wana wa Anaki,

“Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni, watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, NI NANI AWEZAYE KUSIMAMA MBELE YA WANA WA ANAKI? [Kumb 9:1-2].”

FB_IMG_1650478603006.jpg


Mwishowe Yoshua aliwaangamiza wana wa Anaki kutoka katika nchi ya Kanaan, isipokuwa wengine ambao walipata kimbilio katika miji ya Wafilisti ya Gaza, Gathi, na Ashdodi na kujichanganya na kuwa raia wa Ufilisti. (Yoshua 11:22). Na Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mji wa Hebron ambao ulikuwa unakaliwa na wana wa Anaki, hivyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki. [Yoshua 15:14].

Kwa hivyo watu wakubwa huko Ufilisti akiwemo (Goliathi) ambaye Daudi alimuua kwa kombeo alikuwa ni uzao wa Waanaki, Goliathi alikuwa na urefu wa futi 9.8 na alivaa dirii kifuani yenye uzito wa kg 57 na alikuwa na mkuki wenye kg 7. Na mtu mkubwa mwingine katika hao ni Ishi-benobu ambaye uzito wa mkuki wake ulikuwa kg 3.5, huyu pia alipambana na Daudi kiasi cha kukaribia kumuua Daudi, lakini makamanda wa Daudi, (Abishai na Seruya) wakamsaidia na kumuua huyo Mfilisti wa kutisha. Mwingine aliitwa Safu ambaye aliuawa na Sebekai mlinzi wa Daudi katika vita kati ya Waisrael na Wafilisti.

Vita vingine Elhanani kamando wa Daudi alimuua Goliath Mgiti mmoja wa majitu hayo. Huko Gath moja ya mji wa Ufilisti kulitokea vita vingine kati ya Waisraeli na Wafilisti, na Yonathan ndugu wa Daudi alimuua mtu mrefu sana mwenye vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne. Majitu haya manne walizaliwa na mtu mmoja Mrefai ambao wote walikuwa ni masalia wa Waanaki (1 Samweli 17|:1-7; 2 Samweli 21: 15-22). Lakini jamii hii ya magiants ya kina Goliath ilikuwa ni kizazi cha mwisho cha watu wakubwa ambao walichezea kwenye futi 9 na zaidi kidogo, hawakuwa kama baba zao yaani Anaki na Arba babu yao.

FB_IMG_1650478603006.jpg


Mwisho, habari hizi ni za hakika na kweli, mafuvu mengi makubwa huko Kanaani yamevumbuliwa na kutoa hakika ya ukweli huu wa Biblia kuhusu watu wakubwa (Giants) wa kale. Walikuwa ni watu wa kutisha kutoka katika ukoo wa Hamu. Pia habari hii inatufundisha IMANI, kwamba katika Bwana hakuna lisilowezekana, kama Giants waliweza kushindwa ni dhahiri katika maisha hakuna mlima ambao unaweza kuhimili kishindo cha IMANI

Mtoto wa Afrika History.

FB_IMG_1650478599927.jpg

FB_IMG_1650478611524.jpg

FB_IMG_1650478606236.jpg
 
Back
Top Bottom