Watu waliokataa Magufuli asiongezewe Miaka ndio haohao wanashadadia Mbowe aendelee kuongoza. Ndio haohao wanakapinga CCM isiendelee! Unafiki mtupu!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Mpo salama!

Watu wenye ndimi mbili. Watu wenye mawe mawili ya kupimia ni watu Hatari Sana popote walipo. Ni watu wanafiki na muda wowote wanaweza kukuuza.

Alipokuwepo Magufuli, Chawa wake walitoa maoni Yao kuwa Magufuli aongezewe Muda, Magufuli atawale milele, na kama Magufuli angekataa wapo walioapa wangemshikia kiboko kumlazimisha aendelee kutawala. Yalikuwa ni maoni Yao.

Sisi wengine maoni yetu tulikataa tukasema Hapana. Miaka yake ikiisha inatosha. Wengine tukasema Katiba hairuhusu lakini Katiba ni kitabu tuu tunaweza kukibadilisha sehemu ndogo (Constitution amendment) ili kuweka kipengele cha kuongeza Muda.

Haya walewale ambao waliwaka, walimkalia kooni JPM ambaye yeye mwenyewe hata hakuwahi kusema ataongeza Miaka zaidi ya yeye kutamka hataongeza Miaka. Leo hii kile walichokuwa hawakitaki kwa JPM wanakifanya kwenye chama Chao.

Mbowe hata angekuwa kiongozi mzuri kama Malaika, kumuongezea Miaka mingine juu ya ishirini sio Sawa.

Alafu Mbowe angetakiwa aonyeshe uzuri wake katika kuandaa viongozi wengine wazuri zaidi yake wa kumrithi.

Siongei kumtetea Lisu awe kiongozi nope! Anaweza kugombea mtu mwingine Nje ya Lisu na akawa kiongozi wa CHADEMA hii itaonyesha kuwa CHADEMA inaakiba ya kutosha ya viongozi.

Kama kuna watu wanaona Mbowe aendelee Basi wasishangae wale wanaoona CCM iendelee.

Wanasema Mbowe kaitoa CHADEMA Mbali.
Watu wanasema CCM imeitoa nchi Mbali.

Uongozi mzuri ni pamoja na kuweza kuachia nafasi wengine waongoze.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
 
Ndiyo hao hao wakisikia, mama tutamchukulia fomu kwa lazima aongoze awamu ya tatu, watadai demokrasia.
Sijui kwanini chawa wa chadema wanayoyadai kwa ccm na serikali yake hawayataki yatumike kwa chama.
huwa wanahoji kwanini chawa wa ccm husifia kila kitu cha serikali na chama hata kama cha kijinga. Lakini sasa wanapinga kwanini tundu lissu anapingana na mambo ya ajabu yanayoendelea kwenye chama kwamba kwa kufanya hivyo ametumwa, anatumika, hafai, mbowe aliokoa maisha yake n.k.
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
Kwaiyo chama ni Mali ya umma sio kikundi Cha watu wachache na machawa labda muanzishe kikundi Cha kikabila Cha kufa na kuzikana Cha watu wa kaskazini na machawa wenu ila sio chama Cha siasa
 
Kwaiyo chama ni Mali ya umma sio kikundi Cha watu wachache na machawa labda muanzishe kikundi Cha kikabila Cha kufa na kuzikana Cha watu wa kaskazini na machawa wenu ila sio chama Cha siasa
Chama sio mali ya umma, chama ni mali ya wanachama. CHADEMA hakiwajibiki kukidhi matamanio na haja zenu wanaCCM, ACT n.k Kwa mfano CCM wao huwa hawana utaratibu wa kushindanisha nafasi ya mwenyekiti taifa kupitia uchaguzi au kama ambavyo waliamua kutoa fomu moja mwaka 2020 na wameamua kufanya hivyo tena 2025, huo ni uamuzi wa wana CCM, itakuwa kituko CHADEMA kulalamikia huo utaratibu wa CCM au kulazimisha utaratibu wao wanaoona unafaa.
 
Chama sio mali ya umma, chama ni mali ya wanachama. CHADEMA hakiwajibiki kukidhi matamanio na haja zenu wanaCCM, ACT n.k
Naludia tena chama ni Mali ya umma ndo maana wanaokipigia kura chama kwenye uchaguzi wowote ni wananchi wote wewe utakuwa unachanganya kati ya kikundi Cha kufa na kuzikana na chama Cha siasa Kwa maana kwenye kikundi Cha kufa na kuzikana mnazikana wanakikundi tu
 
Hata yanga ikicheza mechi inaangaliwa na watu wote ikiwemo wa Simba, Azam, Tabora n.k ila Yanga ni ya wanayanga.
Kama unafikiri CHADEMA ni mali ya umma nenda wewe mwanaCCM kapige kura za kumchagua mwenyekiti wa CHADEMA.
 
Na ndyo hao hao wanamshangilia Putin na kiduku hawajui utawala wa hawa jamaa ni wa namna gani yaan wanafuata mkumbo tu
 
Kwaiyo lisu anaelalamikia umwinyi uchawa ndani chadema ni CCM nyie machawa wa mbowe mna hoja nyepesi sana
 
Waporaji wa uchaguzi serikali za mitaa wanapotamani Mbowe amwachie Lissu kijiti - kaa chini tafakari kwa kina.
 
Binafsi namshukuru sana Lissu kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CDM taifa, imenisaidia kuwafahamu baadhi ya viongozi waandamizi wa CDM kuwa wapo ki maslahi tu na ni wachumia tumbo tu na wajasilia siasa. Namkubali sana mwamba, lakini kama kweli atagombea tena nitamtoa maana kabisa na nitabadili mtazamo wangu juu ya CDM.
 
Kwaiyo lisu anaelalamikia umwinyi uchawa ndani chadema ni CCM nyie machawa wa mbowe mna hoja nyepesi sana
Lissu ni mwanachadema ana haki ya kulaamikia chochote ndani ya CHADEMA, wewe mwanaCCM huna haki ya kulalamikia chochote ndani ya CHADEMA, unatakiwa ulalamikie mambo yaliyo ndani ya CCM.
 
Hata yanga ikicheza mechi inaangaliwa na watu wote ikiwemo wa Simba, Azam, Tabora n.k ila Yanga ni ya wanayanga.
Kama unafikiri CHADEMA ni mali ya umma nenda wewe mwanaCCM kapige kura za kumchagua mwenyekiti wa CHADEMA.
Narudia tena wewe unachanganya kati ya chama na kikundi Cha kikabila Cha kufa na kizikana harafu usifananishe chama Cha siasa na ushabiki wa usimba na uyanga
 
Lissu ni mwanachadema ana haki ya kulaamikia chochote ndani ya CHADEMA, wewe mwanaCCM huna haki ya kulalamikia chochote ndani ya CHADEMA, unatakiwa ulalamikie mambo yaliyo ndani ya CCM.
Wewe chawa wa Mbowe unakika gani kuwa Mimi ni mwana CCM?
 
Lissu anajua 100% hawezi kushinda, na wahafidhina na wachumia tumbo ndani ya CHADEMA hawawezi kuruhu ashinde.
Lakini kama ataruhusiwa kugombea, au atafanyiwa mizengwe akakatwa atakua ameingia katika vitabu vya kihistoria, na angalau lengo lake moja litakuwa limefanikiwa!
Kumbuka Lissu ni mwanaharakati, wanaharakati lengo lao ni kupaza sauti, sauti ikisikika lengo limetimia!
 
Lissu ni mwanachadema ana haki ya kulaamikia chochote ndani ya CHADEMA, wewe mwanaCCM huna haki ya kulalamikia chochote ndani ya CHADEMA, unatakiwa ulalamikie mambo yaliyo ndani ya CCM.
Lisu yupo clear kabisa na hoja zake Cha ajabu machawa wa Mbowe mmeanza kumuita pandikizi badala ya kujibu hoja zake hivi wewe unatofauti gani na kile kikucha Cha kinamama kinachojiata chawa wa mama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…