SI KWELI Watu wamepigana wakati wa Usaili wa Kada ya Afya nchini Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Watu wanachapana mikono huko, yaani ni noma sana.



Your browser is not able to display this video.

 
Tunachokijua
Usaili wa kuandika katika kada ya afya umefanyika Septemba 3, 2024 nchi nzima ili kuwapta wataalam wa afya watakaojaza nafasi 9, 483 za ajira.

Wakati usaili huu ukiwa unaendelea ilisambaa video mtandaoni ikionesha binti akiwa anasukumwa na Mwanaume akiwa ameshika karatasi kati ya watu wengine walioshika karatasi ndani ya chumba, huku Watu wanaosambaza video hiyo wakidai ni tukio lililotukia kwenye moja ya vituo vya usaili, Tazama( hapa na hapa)

Ukweli ni Upi?
JamiiCheck imefuatilia video hiyo kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Reverse Image ili kufahamu uhalisia wa video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya tukio lililotokea kwenye moja ya maeneo yaliyofanyika usaili katika kada ya afya nchini.

Tumebaini kuwa video hiyo si ya Tanzania na haihusiani na usaili katika kada ya afya, video hiyo ni ya Congo na iliwekwa mtandaoni tarehe Agosti 26, 2024 (Tazama hapa) na kuendelea kusambaa, (tazama hapa) ikionesha tukio lililotokea Congo DRC.

Ufuatiliaji wa kimtandao unaonesha tukio hili lilimuhusisha binti wa chuo cha ISTA Kolwezi lundi (l’Institut Supérieur des Techniques Appliquées (ISTA)) ambaye alishambuliwa na mwalimu akiwa kwenye mtihani Mwalimu anafahamika kwa jina la Tshipamba Kabwe.


Barua ikionesha kusimamishwa kazi kwa mwalimu aliyemshambulia mwanafunzi huyo​
Huyo mwanamme ameshindwa ku control hisia zake mbele ya mwanamke...
Yes wanawake wanatia hasira ila ku deal nao unahitaji uvumilivu hasa upande wa hisia....
Najua hapo huyo mwanamme katukanwa na hako ka dada.
Emotional intelligence ni elimu ya muhimu kujifunza
 
Kuna kipindi katika maisha inahitajika subira ya Hali ya juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…