Konny Joseph
Senior Member
- Aug 28, 2016
- 118
- 199
Ni takribani miaka mitatu sasa CAG amekuwa akitoa taarifa zilizojaa madudu ya ufisadi na rushwa pasi na mamlaka ikiwemo serikali kuchukua hatua yeyeote kukabiliana na tuhuma hizo kwa kipindi chote hicho.
Imefikia hatua sasa wananchi wamepoteza kabisa imani ya kuendelea kusikiliza ripoti hiyo.Mimi binafsi nikiwa mmoja wao sioni kabisa haja ya kuendelea kupoteza mda wangu kusikiliza au kusoma ripoti ambayo kwa ujumla haina tija yeyeote kwa taifa.
Ni wazi kwamba rippoti ya CAG haisomwi ili wananchi wajue tu yaliyomo kwenye hiyo ripoti bali inasomwa ili wananchi wajue pia hatua ambazo mamlaka itazichukua dhidi ya taarifa ya ufisadi itakayowasilishwa katika taarifa hiyo.
sasa kama taarifa zinawasilishwa alafu hakuna hatua yeyote,ni wazi kwamba hatkuna haja ya kuwa hata na hiyo ofisi ya CAG kwa sasa.