Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Watu wanavyosema ajira za serikali zina job security maana yake ni kwamba unaweza kupiga dili na ukajulikana lakini usichukuliwe hatua yoyote.
Hata warning letter hupewi.
Maana kuanzia Mkurugenzi, meneja, mpaka mfagizi na mlinzi wanajuana madili yao.
Sasa wa chini au wa kati akiharibu kwanza bosi anawaza nikimkomalia sana huyu lazima ataibua na mengine akaniharibia.
Pili anawaza ile kibinadamu mbona Mimi mwenyewe nakula kwa urefu wa kamba yangu ngoja huyu nimpotezee tu.
Sekta binafsi mara nyingi mkurugenzi ndiye mmiliki wa kampuni au ndiye mtu ambaye kampuni inamlipa vizuri na kumfanya kampuni aione mali yake. Wa chini au wa kati ukiharibu hawezi kukutupia taulo . Lazima ufukuzwe.