Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 97
- 72
Haamini Kama Kuna Siku ya Kiama
Ukijiona wewe ni kiongozi, na unaona watu unaowaongoza wanalalamikia uvunjifu wa Katiba, kanuni, miongozo, na taratibu ambazo kwa viapo vyako na ahadi yako kwa CCM uliahidi kuvilinda, kuvihifadhi, na kuvitetea, basi fahamu kuwa unafanya kosa kubwa.
Mheshimiwa Rais anasisitiza haki, lakini wewe husikii, umeweka pamba masikioni. Viongozi wa dini wanahubiri haki, lakini wewe husikii. Viongozi wa kitaifa wanahubiri haki, lakini wewe husikii. Umekuwa mkaidi.
Ujue wewe, hata ukitamka neno Mwenyezi Mungu, unajitamkusha tu kutuzuga. Wewe ni tapeli. Upo unasubiri kumaliza tu maisha ya kidunia ili uende zako kuishi motoni. Ndiyo maana hujali vilio vya mafukara, na ndiyo maana ukiona mtu anaandika ukweli, roho yako chafu inakereka.
Bado muda unao. Badilika. Acha kujisahaulisha kwa utamu wa fedha za kuwadhulumu mafukara wanaostahili. Kumbuka daima kuwa moto wa Jahanam kuni zake ni watu na mawe. Na inavyoonekana, usipobadilika na kuacha kufuru, utakuwa mmoja ya kuni za Jahanam.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Mathias Mugerwa Kahinga