Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari za jumapili!
Lisu ni wale watu wasiouogopa ukweli. Watu hao huitwa Jasiri wa asili. Lisu hata akikosea yeye haoni tabu ukimchana makavu na hata yeye kujichana makavu kuwa amekosea. Huo tunaita Uwajibikaji.
Sio rahisi kukemea maovu ambayo hufanywa hata na maboss zako. Sio rahisi.
Ni Kazi ngumu Sana kukemea maovu yanayofanywa na rafiki na watu wako wa karibu. Kazi ngumu Sana.
Lakini kwa upande wa Lisu Jambo hilo kwake sio gumu.
Hii inamfanya asiwe mnafiki.
Watu aina ya LISU sio wazuri Sana ikiwa utakuwa na makandokando yako. Yaani mtu kama Lisu awe Rais wa nchi alafu wewe rafiki yake uwe na makandokando yako. Kwa kweli utakuwa disappointed.
Ni aidha uchague kuacha makandokando au panga la Sheria lipite na shingo yako.
Ukweli ndio demokrasia Halisi.
Kukubali umeshindwa na ulishindwa ni kukubali ukweli na kujipa nafasi ya kuonyesha uwezo na kujipanga upya.
Kuukataa ukweli, umeshindwa lakini unalazimisha ulishinda huko ni kushindwa na kujipanga kulinda kushindwa kwako. Na siku zote utashindwa tuu.
Moja ya vyanzo vikuu vya umaskini, ukandamizaji, rushwa, unyanyasaji, ukatili ni watu kuukataa UKWELI.
Watu wakweli hawawezi wakandamizaji, Wala rushwa, wanyanyasaji na wakatili.
Hata kwenye masuala ya kifamilia, ukandamizaji wa Haki za wanawake au watoto mara nyingi chanzo chake kikuu ni kuukataa UKWELI.
Mauaji ya wanandoa, Mume kumuua mke, mke kumuua Mume. Mume kumpiga Mke ni MATOKEO ya watu kukataa UKWELI.
Watibeli tunaujua ukweli na kuupenda.
Huwezi kumlazimisha Mkeo aache kuku-cheat wakati ukweli ni kuwa yeye anapenda kufanya hivyo. Lazima ukubali ukweli kuwa Mkeo anapenda kufanya ngono na wanaume wengine. Ukweli huo utakupa maamuzi ya kweli na HAKI. Utaamua umuache kwa Talaka, au kama moyo wako hauwezi kumuacha Basi uishi naye vivyohivyo na Tabia zake Mbaya.
Utekaji, mauaji yaliyotokea nchini, ambayo yanahusishwa na Siasa ni MATOKEO ya kuwa na watawala wasioukubali UKWELI na wasiotaka kuufuata. Matokeo yake huwa ni dhulma kubwa ya kupoteza Maisha ya watu au kuyajeruhi.
Mtu Fulani anaposema na kuikosoa serikali au kumkosoa mtawala au kumtukana Kabisa. Lazima mtawala au watawala wakubali ukweli kuwa watu wako tofauti na nihaki ya asili watu kutofautiana.
Ikiwa Sheria zitavunjwa na utofauti huo wa asili basi lazima Sheria zitumike kuadhibu wafanya makosa.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam