GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Ninazungumzia baadhi ya wenzetu humu jukwaani ambao ama sijawaelewa, au wana "tatizo".
Nimeliona hili pindi mtu anapouoandisha uzi ambao una chembe za kifursa. Mathalani , mtu anaweza akawa anaelezea fursa zinazopatikana kwenye shughuli fulani kama kilimo, biashara, n.k.
Imeshuhudiwa mara nyingi kuwa nyuzi kama hizo hukutana na miitikio tofauti. Kuna wanaoziunga mkono, na hata kuchangamkia fursa iliyoelezewa, na wengine huziponda, kana kwamba ni kitu kibaya.
Wanaopinga, mara nyingi wanaonekana kuwa na mashaka kuwa mtoa mada anataka kufanya utapeli au anataka kujinufaisha kupitia uzi huo.
Tuchukulie basi kuwa mtu anataka kujinufaisha kwa kutangaza biashara yake kupitia JF, atakuwa amekosea? Kama amevunja kanuni za jukwaa, si kuna utaratibu wa kumripoti kwenye mamlaka husika? Kwa nini mtu apoteze muda wake kumkejeli au kuwavunja wengine moyo kuhusiana na kinachoelezwa na mtoa mada?
Kwa nini watu wanakuwa waoga sana, na kuishi katika hali ya mashaka kiasi hicho?
Wanafahamu kuwa hilo nalo ni tatizo la Kisaikolojia?
Simaanishi watu wasichukue tahadhari, la hasha! Kuchukua tahadhari ni muhimu. Lakini mtu anayechukua tahadhari mithili ya mchezaji ambaye kazi yake kubwa ni kuzuia kufungwa, si rahisi kufanikiwa.
Huwezi kufunga goli ikiwa hutaki kucheza mbali na goli lako kwa hofu kuwa adui yako atapata nafasi ya kukufunga. Ni sahihi kulilinda goli lako, lakini usiache kulishambulia goli la adui. Ni lazima kukubali "kutake risk" kwa kutoka langoni kwako ili uweze kutia mpira kwenye lango la adui yako.
Usimwamini kila mtu kizembe, lakini pia ni vigumu kufanikiwa maishani endapo hutawaamini watu wengine.
Kwa mtazamo wangu, ninaweza nikasema watu wenye tabia hizo wanaweza wakawa na mojawapo ya matatizo yafuatayo(wanaweza, simaanishi kuwa wanayo):
1. Ni wabinafsi sana kiasi kwamba hawataki wengine wafanikiwe kama wao au kuwazidi wao!
2. Ni waoga sana
Labda alishawahi kutapeliwa au anamfahamu mtu aliyetapeliwa, hivyo anajitahidi kuchukua tahadhari asije akaanugukia kwenye huo mkenge. Kwa mtu aliyewahi kugongwa na nyoka, akiguswa na kijiti, akili yake hukimbilia kuhofia kuwa kagongwa tena na nyoka.
Mtu aliyeathiriwa na hiyo hali ni mgonjwa Kisaikolojia. Anatawaliwa na taarifa hasi. Anastahili kusaidiwa.
3. Wamekata tamaa
Kwa jinsi wengine wanavyochangia, ukitazama kwa hicho la Kisaikolojia, ni kama vile watu waliojikatia tamaa. Kwa mtu aliyekata tamaa, kwake yeye hakuna lililo jema. Ni vigumu kuona jema hata awapo katikati ya Ziwa la mema
4. Inferiority complex!
Wahenga walisema, "kifo cha wengi ni harusi". Kwa mtu aliye na tatizo la inferiority complex, labda ya kiuchumi, huwa na tabia ya kuhofia mafanikio. Wanasaikolojia wanalifahamu hilo.
Kama mtu, kwa mfano, ana umaskini wa ndani (subconscious mind), akili yake itajitajitahidi kumkwamisha kuipokea fursa yoyote inayoweza kumkwamua kutoka katika hali duni. Hakusudii, bali akili yake ya ndani (subconscious mind) humwamuru kuchukua maamuzi yatakayomwepusha kutoka katika hali duni.
Si hivyo tu, bali pia itamwelekeza jinsi ya kuwazuia watu wake wa karibu "wasimtoroke" kutoka katika hali duni. "Furaha" ya watu wenye huo "ugonjwa" ni kuona kuwa si yeye peke yake aliye na hali duni. Kwa hiyo, ikitokea kuna mtu anataka kuchomoka kutoka katika hali duni, huweza kumshauri vibaya au kumkatisha tamaa asichukue hatua itakayomfanya watengane. "Subconscious mind" yake inafahamu kuwa endapo huyo rafiki yake atafanikiwa, urafiki wao utakufa.
Na, mtu anapofanya hayo, hakusudii, bali ni hali ambayo inamtawala bila yeye kujua.
Kutokana na mijadala niliyoiona humu, ambapo wakati mwingine mtu anaweza akawa ameupandisha uzi ambao kuna watu wangenufaika nao, au wanaonufaika nao, lakini ghafla tu wanatokea watu wengine na kuanza "kucomment negatively", ninashawishika kufikiri kuwa inawezekana baadhi ya wenzetu humu jukwaani hawako sawa Kisaikolojia .
Ushauri wangu ni kuwa kama mtu unajua una tatizo la kuwa na mtazamo hasi, ni bora kutafuta msaada kwa wataalam. Vinginevyo, unaweza ukajikuta unaendelea kujiathiri bila wewe kujua, na hata kuwaathiri watu wako wa karibu. Kama ni mzazi na una tatizo hilo, ni rahisi kuwaathiri hata watoto wako na hivyo kuharibu kesho yao.
Nitolee mfano wangu binafsi. Nilikuwa na tatizo la kuogopa sana vyombo vya moto, hasa pikipiki na gari. Ilikuwa ni kawaida kuruka pindi gari au pikipiki inapokaribia mahali niliko. Nilikuwa naona kama vile dereva anataka kunigonga. Wakati mwingine nilikuwa nikiruka mpaka watu wananishangaa.
Sikuipenda hiyo hali, na wala sikuijua chanzo chake. Ni mpaka mwaka 2018 nilipokuja kubaini chanzo chake na hivyo kutafuta suluhu. Ilinichukua siku chache sana, nafikiri wiki moja, "kupona", baada ya kufahamu chanzo cha hilo tatizo.
Siku hiyo, mwaka 2018, nilikuwa katika tafrija fulani, na nikawa nimekaa meza moja na watu wawili ambao walikuwa na utaalam na masuala ya saikolojia. Mmoja alikuwa mhadhiri wa Saikolojia katika Moja ya Vyuo Vikuu jijini Nairobi, Kenya.
Miongoni mwa story zilizokuwa zinetawala mezani hapo, ni stori za Kisaikolojia. Kuna mada moja ilizungumziwa na ikanifungua macho kuwa na mimi nilikuwa "mgonjwa".
Siku hiyo nilifahamu kuwa kilichokuwa kikinifanya noyaogope magari ni tukio lililotokea mwaka 2001. Mwaka huo, 2001, nilipata ajali ya kugonga gari, mimi nikiwa ninaendesha baiskeli. Baiskeli haikuwa na breki, nikajikuta nimelinyooshea gari lililokuwa linakuja mwelekeo wangu. Bahati nzuri, dereva alivyoona ninaenda kumgonga, alisimama.
Nakumbuka, baiskeli yangu iliparamia gari kwa mbele, Mimi nikalala juu ya boneti la gari huku baiskeli ikiangukia mtaroni. Sikuumia sana, lakini nilishtuka sana.
Watu walipokumhia kuja kunisaidia, walipokuwa wakiniongelesha, sikuwa nikiwajibu japo nilikuwa nikiwasikia. Ilinichukua muda kuja kuanza kuongea, na ni baada ya mtu mmoja kushauri kuwa niachwe kwanza nipate utulivu.
Kumbe, hiyo ajali ulipeleka taarifa hasi kwenye akili yangu ya ndani kuwa vyombo vya moto vinavyotembea ni hatari kwangu. Ndiyo maana nilikuwa nikivikimbia.
Nilipolifhamu hilo, niliwauliza hao wataalam jinsi ya kuondokana na kadhia hiyo. Nilipofahamu, nilifanya kama nilivyoelekezwa na hatimaye nikawa huru baada ya "mateso" ya maiaka kumi na saba.
Usiuonee ugonjwa aibu! Kama una hilo tatizo, tafuta ufumbuzi haraka.