Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Salaam ndugu zangu,
Katika pitapita zangu za hapa na pale nimekutana na watu adhaa wakanionya kuwasaidia watu naokutana nao njiani na kunisisitiza kuwa makini.
Wadau wanasema kwamba watu wengi wanaomba mijini hawafanyi hivyo kwa ajili yao bali kuna baadhi ya watu wenye vipato vikubwa ambao wanawatoa watu vijijini kisha kuwafanya ombaomba na jioni wanapeleka hesabu.
Inaelezwa kuwa watu hao pia wamewakusanya na kuwaajiri watu kwenye biashara za karanga na mayai kisha jioni wanaenda kupeleka hesabu.
Je, kuna ukweli katika hili?
Kama kweli je vyombo vya usalama vinakwama wapi kuhakikisha wanazuia watu kufanywa bidhaa?