Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Hivi karibuni kama mmefatilia kwenye matukio haya ya kupotea/kutekwa na watu wasiyojulikana mtagundua kuna kitu, kuna pattern inatengezwa kuisafisha serikali na vyombo vya ulinzi, kwa kufanya kuwa wote waliotekwa wameamua kujificha wao wenyewe kutokana na sababu mbalimbali. Wakienda mbali sana ni kuhusisha matukio hayo na ajali.
Na kama mmefatilia katika matukio haya yote maelezo ya polisi hayaeleweki, na kesi zinayeyukia juu kwa juu utafikiri hakuna kilichotokea!
Picha limeanza kwa Mkurugenzi wa Dar24, akatekwa na kupatikana tukaambiwa ni mambo ya biashara na waliomteka anawajua. Kesi imeishia wapi mpaka leo, mimi na wewe hatuna majibu!
Tukio la bonge Tarimo the same, tena lilikuwa sooo sloppy, wakawatumia watu wanaojulikana, tena waonekane kwenye kamera, hapa pia tukaambiwa ni mambo binafsi ya kibiashara, mtangazaji akawa anatumia muda mwingi kweli kudirect maswali kwa serikali na polisi ili isemwe kuwa hawahusiki. Bonge mwenyewe kutoka stori za mtaani ni mafia mzuri tu, dili zake zinajulikana vilivyo huko 'ngazini juu'. Millard Ayo alivyoripoti tukio hilo na kimbelembele kwenda kumhoji jamaa nikajua hapa kuna jambo. Wamekamatwa, kesi inaendelea kimya kimya hatupati updates, na lenyewe litaenda shwaa kama ilivyokuwa kwa Mkurugenzi wa Dar24.
Tukaja kwa jamaa aliyekutwa kwa mganga ikisemekana alikimbia madeni, kuna yule mwingine ambaye alikuwa polisi; bwana Ulomi, tukaletewa picha haeleweki kuwa alipata ajali na mwili ulipelekwa polisi kama mtu asiyejulikana, huku toka jana yake taarifa ikiwa imepelekwa polisi kuna mtu kapotea

mapichapicha!
Likaja tukio la Abdul Nondo, hapa ikawa tofauti kidogo, this time aliyepotea/tekwa si mfanyabiashara, ni mwanasiasa! Wakamchakaza kidogo naye wakaenda kumuacha Coco Beach ili 'wasamalia' wampate na kumpeleka hospitali. Akiambiwa acha kupiga kupiga kelele, acha chokochoko tutakuua! Hawakutaka kumuua in the first place! Waliokamatwa wote walikuwa hawana connection na siasa, ilibidi wabalance shobo kwa Nondo! Nako Millard yule akakimbia chap kwenda kumhoji, nako tulipata ujumbe.
Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Jana tumepewa taarifa nyingine ya mwandishi wa TV3, kituo chake cha kazi kikaripoti kuwa hajulikani alipo tukaja kuambiwa alikuwa kwa shangazi yake
Leo tumepata fungakazi ya fungua mwaka! Millard Ayo karipoti mfanyakazi wake hajulikani alipo, na hii ni baada ya siku 9 toka kutoweka. Najua Wakuu mnafikiria kama nnachofikiria, Millard Ayo huyu huyu anayetumika na kila mafia na wachafu hapa nchini ili awasafishe, kijana ambaye hana lolote atekwe kabisa?!🌚🌚🌚 Stori itakuwa ile ile nawaambia.
Sitashangaa Soka na wenzake wakipatikana tukaambiwa waliamua kujificha sehemu fulani (au tutatengenezewa stori kabambe ya ajali ya kumezwa na samaki wakafa 🌚) ili CHADEMA ipate umaarufu na CCM, Serikali pamoja na Jeshi la Polisi waendelee kuchafuliwa. Pia ripoti ya Ali Kibao itakuja na matobo ambayo hata mtoto wa primary atashangaa! Utatolewa mkwara mzito kwa wananchi kuacha kufanya matukio haya and everibody atakuwa hapi!
Namna hiyo Serikali, CCM na Polisi watakuwa wamesafishwa, kwenye kampeni wimbo utakuwa mmoja tu "Mama amekomesha Utekaji, ona wakina Soka walikuwa hawajatekwa ni kuichafua tu serikali", uchaguzi mambo yawe bull bull.
There are no coincidences! Mtarudi kwenye huu uzi karibuni.
Hivi karibuni kama mmefatilia kwenye matukio haya ya kupotea/kutekwa na watu wasiyojulikana mtagundua kuna kitu, kuna pattern inatengezwa kuisafisha serikali na vyombo vya ulinzi, kwa kufanya kuwa wote waliotekwa wameamua kujificha wao wenyewe kutokana na sababu mbalimbali. Wakienda mbali sana ni kuhusisha matukio hayo na ajali.
Na kama mmefatilia katika matukio haya yote maelezo ya polisi hayaeleweki, na kesi zinayeyukia juu kwa juu utafikiri hakuna kilichotokea!
Picha limeanza kwa Mkurugenzi wa Dar24, akatekwa na kupatikana tukaambiwa ni mambo ya biashara na waliomteka anawajua. Kesi imeishia wapi mpaka leo, mimi na wewe hatuna majibu!
Tukio la bonge Tarimo the same, tena lilikuwa sooo sloppy, wakawatumia watu wanaojulikana, tena waonekane kwenye kamera, hapa pia tukaambiwa ni mambo binafsi ya kibiashara, mtangazaji akawa anatumia muda mwingi kweli kudirect maswali kwa serikali na polisi ili isemwe kuwa hawahusiki. Bonge mwenyewe kutoka stori za mtaani ni mafia mzuri tu, dili zake zinajulikana vilivyo huko 'ngazini juu'. Millard Ayo alivyoripoti tukio hilo na kimbelembele kwenda kumhoji jamaa nikajua hapa kuna jambo. Wamekamatwa, kesi inaendelea kimya kimya hatupati updates, na lenyewe litaenda shwaa kama ilivyokuwa kwa Mkurugenzi wa Dar24.
Tukaja kwa jamaa aliyekutwa kwa mganga ikisemekana alikimbia madeni, kuna yule mwingine ambaye alikuwa polisi; bwana Ulomi, tukaletewa picha haeleweki kuwa alipata ajali na mwili ulipelekwa polisi kama mtu asiyejulikana, huku toka jana yake taarifa ikiwa imepelekwa polisi kuna mtu kapotea

mapichapicha!Likaja tukio la Abdul Nondo, hapa ikawa tofauti kidogo, this time aliyepotea/tekwa si mfanyabiashara, ni mwanasiasa! Wakamchakaza kidogo naye wakaenda kumuacha Coco Beach ili 'wasamalia' wampate na kumpeleka hospitali. Akiambiwa acha kupiga kupiga kelele, acha chokochoko tutakuua! Hawakutaka kumuua in the first place! Waliokamatwa wote walikuwa hawana connection na siasa, ilibidi wabalance shobo kwa Nondo! Nako Millard yule akakimbia chap kwenda kumhoji, nako tulipata ujumbe.