Watu wanatekwa na kuuawa mnakaa kimya kwakuwa sio wanachama wenu wala ndugu zenu, watu wenu wakiguswa kidogo tu mnatoa matamko usiku usiku

Watu wanatekwa na kuuawa mnakaa kimya kwakuwa sio wanachama wenu wala ndugu zenu, watu wenu wakiguswa kidogo tu mnatoa matamko usiku usiku

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Nimeliona bandiko la ndugu yetu Mwigulu Nchemba, ambaye hajawahi kutoa tamko lolote kuhusu watu wanavyotekwa na kupotezwa, labda kwa sababu sio wanachama wao au ndugu zao. Hali hii inaonyesha ulevi wa kupindukia wa madaraka. Jana, baada ya watu wao kuguswa kidogo, amekurupuka kutoa matamko.

Swali ni, lini TRA hukamata magari kwa kuyakimbiza barabarani? Na kuhusu gari lenye namba "D," limekuwaje hadi leo halijakamatwa? Kwa nini msiwatumie trafiki kukamata gari hilo, ilihali mnazo namba zake? Pia, gari hilo lilitokaje bandarini na namba za usajili zilitolewa vipi?

Ni vyema kuacha kutetea wauaji na kuwavisha mavazi ya wafanyakazi wenu. Nasema tena, hawa wameguswa kidogo sana.
 
Na bado, tutaelewana. Wakijichanganya wawe wananyooshwa tu.
 
Idara yake inayomkusanyia feza imeguswa, ukute hata hizo hela zisingefika zingeishia mifukoni mwao.
 
Back
Top Bottom