Naomba kuuliza jamani, hivi hawa watu wanaotaka watu wa like na kushare picha zako na kuwalagai kwa zawadi ambayo ukweli hawazitoi, wana mlengo gani? Hivi wanawaona watu ni wajinga sana kwa kudanganyika na vizawadi visivyokuwa ba mbele wala nyuma.
Hasa wasanii wa kibongo. Kila wakitupia picha zako mtandaoni. Utasikia ukilike na kushare picha hii utapata zawadi ya simu. Kwani wanafikiri watu hawana simu?
Hivi ni faida gani anayopata mtu endapo picha aliyoweka mtandaoni italikiwa (liked) na kushared (shared) na watu wengi?