Dusabimana
JF-Expert Member
- Oct 24, 2019
- 278
- 248
Kama kichwa cha Habari ulivyo soma hapo juu.Ni kwamba kuna changamoto katika utoaji wa Vitambulisho vya Taifa,hasa kwa Mikoa inayo pakana na Nchi jirani. Mfano ni Mkoa wa Kigoma, unakuta baadhi ya Watu wana wamiliki Warundi kwa miaka mingi na kuwafanyisha kazi za Majumbani,Mitaani na Mashambani.Tatizo linapo kuja ni kwamba hawa Warundi baadhi yao wameingia Nchini bila Vibali au kufuata utaratibu unao takiwa kisheria.Suala jingine ni hao Warundi kujisajili katika mazoezi mbalimbali likiwemo na hili la NIDA ambalo baadhi yao walishiriki kwa udanganyifu. Wameenda katika Vituo vya kusajili wame andikisha mwanzo Majina yao halisi, lakini ya Baba zao au Majina ya Ukoo wao wamedanganya kwa kuandikisha ya Mabosi wao wanaowafanyisha kazi na kuwahifadhi! Na hao Mabosi wao huwezi sikia wakiwazuia kujisajili wanapiga kimya tu, sana wakikwaluzana ndo utasikia Murundi anapigwa mkwala! Maoni yangu ningeomba Mamlaka zinazo husika wangelitazama suala hili kwa umakini kwa kushirikiana na Viongozi wa Mitaa kuwabaini hawa Wahamiaji haramu,kabla ya kukabidhi Vitambulisho vya NIDA kwa Wananchi.