Watu watafurahia ukianguka kiuchumi

Watu watafurahia ukianguka kiuchumi

Bahati mbaya waafrika ni jamii chache sana zenye hurka za kusaidia wenzao.

Yaani ni ukweli ulio wazi sisi ni full nongwa uanguke na watu wanashangilia, japo hutawaona na hii haijalishi sijui kanisani hama msikitini.

Ni mmoja katika watu 75 ndiye atauzunika na kukufariji.
 
Habarini wakuu

Husika na kichwa cha habari.

Hakikisha unafanya kazi kwa bidii uenda umejiajiri au umeajiriwa hakikisha akili yako inaamka mapema kimaendeleo wekeza ( invest ) pesa yako sehemu husika na uwe na tabia ya kuhifadhi pesa kama hakiba, fungua biashara ndogo ndogo unazoziweza na ajiri watu wasimamie biashara zako na hakikisha unafanya kazi kwa bidii na unapanga malengo na mda hayo malengo wa kuyatimiza. Kama hauna uchumi wa kutosha weka nia ya mambo hayo kama utakuja kupata, watu watafurahi anguko lako kiuchumi watakucheka siku ukikosa mahitaji yako muhimu hakikisha hata ukianguka hawajui kama umenoa.

Uenda ulikuwa unawasaidia ulipokuwa na uchumi mzuri pamoja na hayo bado watafurahi, uenda ulikuwa ukiishi nao na wanakupa moyo kuwa endeleza mapambano na kusema nakuona mbali sana miaka kadhaa ijayo na bado watafurahi na kukucheka anguko lako la kiuchumi na wapo pia ndugu zako wa karibu pia watafurahia anguko lako kiuchumi bila sababu yeyote ile, weka hakiba sana wekeza pesa zako mahala husika, anzisha biashara tofauti tofauti kama hauna mtaji mkubwa anzisha biashara ndogo ndogo, hakikisha haudondoki kama zigo la kuni kiuchumi. Ukianguka taratibu utaweza ukainuka bila maumivu na kupata nguvu ya kuendelea bila yeyote kujua ila usiache kuwasaidia hata kama unafahamu kuwa ukija kuanguka kiuchumi watafurahia.

Asante
Yeap[emoji123]
Hili jambo nasemaga kila mara ni vyema kuishi maisha ya kutoeleweka kwamba ukipata pesa watu wajue ukiishiwa watu wanajua kwakua kuna namna umejiweka ukizipata unakua namna gani na zikiisha unakua namna gani usisomeke yani ziwepo zisiwepo wasijue,
Sio mwingine akizipata analewa mchana mpaka usiku ye ni kunywa tu ata job aendi zikiisha alewi anaanza kwenda na job washajua zimeisha[emoji1787]
 
Back
Top Bottom