Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilya amesema kupitia Operesheni iliyofanyika hivi karibuni Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu (3) wote wakazi wa Dar-es- Salaam wakiwa na jumla ya simu 79 ambazo waliziiba katika Tamasha la Wasafi Festival lilifonyika Songea tarehe 16.09.2023.
Amesema kati ya simu hizo 50 zimetambulika na kukabidhiwa kwa wahusika na simu 29 ambazo ni, Ifinix 04, Tekno 09, Sumsung 04, Google pixel 2, Iphone 1, Huwawei 1, Oppo 1, Itel 1, Nokia 3 na simu ndogo (Viswaswadu) 3 na Mashine moja yakusajilia line za airtel na Laptop moja aina ya Acer bado hazijatambulika.
Jumla ya watuhumiwa 20 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria
Amesema “Sambamba na hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru tumeendesha Operesheni kali ya kuwaondoa wafugaji wote ambao walikutwa wakiendesha shughuli za ufugaji katika maeneo ambayo siyo rasmi kwa ufugaji.
Ameeleza kwa kipindi cha kuanzia tarehe 17/09/2023 hadi tarehe 23/10/2023 cha Oparesheni hiyo tumefanikiwa kuwakamata wafugaji 81 wakiwa na Jumla ya N’gombe 12,622 katika maeneo yasiyo rasmi kwa ufugaji na kutozwa faini ya Tsh. 297,168,000= (Shilingi Milioni miambili tisini na saba, Laki moja na Sitini na nane elfu) kwa mujibu wa Sheria za Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambazo ni, Sheria ndogo ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru GN 31 ya 2005, Sheria ya Mazingira NA.20 ya 2004 na Sheria ya mpango wa matumizi bora ya ardhi NA.6 ya 2006 na fedha hizo kuingizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, na wafugaji wote waliotozwa faini walipewa Stakabadhi ya EFD Machine.
Aidha, kufuatia Operesheni hiyo Wilaya ya Songea kwa vipindi tofautitofauti Polisi wamekamata jumla ya Ng’ombe 136 zilizokuwa zimeingizwa\ Mkoa wa Ruvuma bila kufuata taratibu za kisheria na kutozwa ya faini ya pesa za kitanzania Tsh.1,960,000/ (Shilingi Milioni Moja Laki tisa na Sitini elfu) kisha Kuamriwa Ngombe hizo kurudishwa mahali zilipotoka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilya