Watu wengi sana wamepumzisha Mabanda yao ya kuku na Mashine za Kuangulia

Kitu ambacho tunatakiwa kujiuliza unapoanza mradi wowote ni je unauelewa was kutosha kuhusiana na huo mradi wako?
Watu wengi tunaingia kwenye miradi hii kwa sababu ya mihemko ya kuona mtu fulani kafanikiwa ngoja na Mimi nifanye hapo ndipo tatizo linapotokea.

Nilianza kufuga kuku 2014 hawa hawa chotora aina ya sasso sijawahi kupoteza kuku zaidi ya mmoja au wawili tena kwa kulaliana.

Sijasomea wala sina elimu ya mifuga lakini nilijifunza kutoka kwa mtaalamu wa mifugo ambae nae alikuwa anafuga.

Ngoja niwambie kitu kimoja muogope sana afisa mifugo ambae amesomea kwenye makaratasi hata kuku mmoja hana atakushauri vitu vingi sana ambavyo hata wewe utachanganyikiwa. Za kuambiwa changanya na zako.

Kuku wanalipa fuga kuku kwa malengo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wengi tunaingia kwenye biashara kwa sababu tunaona fulani kaingia na siyo kwa sababu tuna ujuzi nayo. Hilo ndilo kosa la kwanza. Na tukianza kuigana tunaigana kweli kweli utafiria ni sheria imepitishwa lazima kila mtu afanye hiyo biashara. Ufugaji wa kuku unatakiwa mtu ajindae, awe na capital ya kutosha na asifanye mambo kama ilivyozoeleka.

Hivi kwa wale wenye mtaji wa kutosha kuna umuhimu gani wa kuuzia kuku wako hawa wateja magumashi wanaokuja mmoja mmoja? Tujari kuwaza nje ya box jamani. Kwa nini mfugaji asijenge sehemu aweke mafriji na kuku wanapofikia muda wa kuuza anawachinjwa na kuuza mwenyewe kwa bei rahisi? Tena mtu anaweza kwenda mabali zaidi na akawa anatenga mapaja peke yake, vipapatio peke yake, vidari peke yake nk na kupack kwenye mabox kama wanavyofanya majuu.
 
Kwa wale tunao anza tuna la kujifunza hapa jifunze kwa walio fanikiwa keep that passion,tuache kukatishana tamaa kila biashara inachangamoto hakuna jambo jepesi tufuate taratibu na miongozo ya ufugaji & Trust the process.
 
Umenirudisha kwenye reli, Kwa sasa mambo yakoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwanini mnahasi wanyama ili kukidhi tamaa zenu za kibinadamu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sawa na biashara ya daladala huna moyo huiwezi
 
Mimi nimeamua kuingia fully yaani kufanya eco system kabisa,nalima mahindi,mpunga, alizeti nipate pumba na mashudu huku nafungua mashine ya kusaga nategeneza kabisa chakula cha kuku then natengeneza mbolea napeleka shambani kwa ajili ya mimea
 
Nifungue kuhusu changamoto ya chakula.
 
Nifungue kuhusu changamoto ya chakula
 
Afisa mifugo alikuja kuwakata midomo kuku wa mayai (layers), naamka asubuhi kuku zaidi ya mia wamekufa, yaani wengine alikuwa anakata hadi ulimi. Kwa sasa nafanya mweyewe baada ya kujifunza na kununua ule mkasi maalumu wa kukatia.
 
Afisa mifugo alikuja kuwakata midomo kuku wa mayai (layers), naamka asubuhi kuku zaidi ya mia wamekufa, yaani wengine alikuwa anakata hadi ulimi. Kwa sasa nafanya mweyewe baada ya kujifunza na kununua ule mkasi maalumu wa kukatia.
Alikulipa hiyo hasara sasa, such alikijibu Vip baada ya kumwambia kuhusu hilo
 
Afisa mifugo alikuja kuwakata kidomo kuku wa mayai (layers), naamka asubuhi kuku zaidi ya mia wamekufa, yaani wengine alikuwa anakata hadi ulimi. Kwa sasa nafanya mweyewe baada ya kujifunza na kununua ule mkasi maalumu wa kukatia.
Alikulipa hiyo hasara sasa, such alikijibu Vip baada ya kumwambia kuhusu hilo
Hakulipa chochote, ni vijana waliomaliza vyuo vya mifugo wako mtaani wanabangaiza.
 
Familia yangu inafuga kuku wa nyama kuanzia mwaka 2008 na mradi unasimamiwa na mke wangu. Changamoto ni nyingi sana kama masoko na magonjwa.

Kuna kipindi waliwahi kufa kuku wote katika mabanda matatu na tukakaa miezi minne bila kufuga ila baadae tukaendelea tena. Cha muhimu ni kujua magonjwa na kuwakinga mapema na pale ugonjwa unapotokea unautafutia tiba haraka. Pia ujenzi wa mabanda ni kitu cha kuzingatia ili kuwaepusha na magonjwa kama mafua. Usafi wa mara kwa mara pia ni muhimu sana.

Kwa DSM wateja sio issue ila tatizo ni wateja kuwalalia wafugaji pale kuku wanapokuwa wengi sokoni. Binafsi ufugaji kuku umetusaidia sana katika maisha yetu. Sie tuna mitaji mitatu ya kuku elfu moja elfu moja na kuna mabanda makubwa mawili na moja dogo la kuanzishia, kwa mwezi tunauza kuku elfu mbili. Kuna kipindi cha changamoto na kipindi cha mavuno mazuri haswa.

Unatakiwa kuwa na akiba benki ili ikija changamoto usidondoke mazima. Biashara yoyote ina ugumu na hizi za viumbe hai ni changamoto zaidi. Uzuri wake ni kuwa haina kodi yoyote

Pia aina ya chakula ni muhimu sana kwani kuna baadhi ya vyakula vinaweza visinenepeshe vizuri. Na pia unatakiwa usiwe bahili kwenye kulisha lakini ufanye timing ya muda wa kuwatunza. Pia utakiwi kukata tamaa kwenye biashara ya kuku. Mke wangu ameanza toka 2008 na mpk leo anaendelea
 
Ufugaji, Ukulima, Kuuza vitu vinavyoharibika ndani ya siku 7 hapana kabisa
 
Brother u
 
Mradi wa ng'ombe unaendeleaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Niombee formula ya utengenezaji chakula kwa shemeji Mkuu wangu Kama hutojali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…