Watu wenye jinsia mbili ni kama Serikali imewasahau kuwasaidia

Watu wenye jinsia mbili ni kama Serikali imewasahau kuwasaidia

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Serikali ina wajibu kumuangalia kila mwananchi wake sehemu mbalimbali. Ila watu wenye jinsia mbili ni kama serikali imewasahau na kuwatelekeza kabisa.

Mara ya kwanza sikuwa naelewa kuhusu ili swala mpaka nilipoweza kuona makala BBC swahili ikieleza changamoto wanazopitia tokea wadogo mpaka ukubwani.

Changamoto wanazopatika ni kushindwa kueleweka yeye yupo upande gani wa kiume au wakike sababu maumbile yote yapo.

Suala la kibailojia kwenye mwele kutokubalika kwenye makundi mawili jinsia hizo mwisho wasiku ujiona sio kama binadamu wakawaida.

Kuchekwa au kunyanyapaliwa pindi ajulikanapo. Kwenye swala kwili kuna wengine ambao sehemu zote mbili hufanya kazi na wengine moja hufanya au kutofanya.

Soma pia: Masaibu ya kuzaliwa na jinsia mbili

Je, serikali imeliangalia vipi ili suala? Inawezekana tunaona wengi na wengine wakishiriki mijadala kwenye mitandao ya kijamii wakashindwa kujieleza au kutotambulika.

Kuhusu nchi yetu kuwa na watu wenye imani potofu; unalichukulia vipi kama mtoto akizaliwa wa aina hii?

Tunaweza jadili
 
Tuseme na wewe mleta mada unazo jinsia mbili?

Hayo mambo yalitakiwa yabainishwe na wakunga.

Unapojifungua wao ni wa kwanza kumgagua mtoto, sijui kama miaka hii wakunga wapo makini tena.
 
Wako wangapi? Unataka serikali iwafanye nn? Vitu vingine bhn ni mzigo, serikali iache kufanya vitu vya maana ianze kuwaza nyeti zako
 
Mi nilidhani wewe ndio ungetuambia serikali iwafanyie nini? Wewe ndio umeibua hili suala kwahio tuambie changamoto zao ni zipi na na serikali inatakiwa ifanyeje kuwasaidia
 
Tafuta movie inaitwa 20,000 Species of Bees, humo wazazi wanapata mtoto mwenye changamoto hio yaan transgender, wao wazazi wanataka mtoto awe wa kiume wakaanza kumtreat km mtoto wa kiume Ila alipofikisha miaka 8 mtoto akaanza kujitambua kua yeye sio mtoto wa kiume bali yeye ni mtoto wa kike pamoja na kwamba ana vifaa viwili huko chupini
 
Yaani kwamba serikali haitoki hadharani kuufahamisha umma kuwa kuna watu wenye wanazaliwa na jinsia mbili na hakuna namna ya kubadilisha, badala yake wanaweza kuzifanyia kazi tu zile wanazotaka. Kwa hivi jamii itakuwa na ufahamu kuhusu hawo watu, maana jamii ina mtizamo wa kuwa ukiwa na jinsia mbili ni kosa au dhambi.
 
Jinsia mbili zote haziwezi kufanya kazi sahihi lazima moja inakua haifanyi kazi, kwahiyo serikali unataka iwakusanye iwafanye nini?
 
Tuseme na wewe mleta mada unazo jinsia mbili?

Hayo mambo yalitakiwa yabainishwe na wakunga.

Unapojifungua wao ni wa kwanza kumgagua mtoto, sijui kama miaka hii wakunga wapo makini tena.
Kuibua hoja na matatizo sio kigezo kuwa wewe ndio muhusika.

Tuwaelezee wasipingwe na wachukulie ni watu.kila mtu ana haki ya kusemezewa.

Nikiwatetea albino sio kwamba ni albino.

Nikiwatetea walemavu sio kwamba mimi ni mlemavu.

Nikiwatetea wapatao shida huko syria,lebanon,congo na n.k sio kwamba mimi ni raia wa huko.
 
Hivi wale transgender ni watu wanakuwa wamezaliwa na jinsia mbili kama hawa unaowaelezea au ni vipi
 
Back
Top Bottom