Watu wenye majina makubwa kuliko kazi zao!

Mkalibari

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2012
Posts
659
Reaction score
399
Kuna baadhi ya watu maarufu ndani na nje ya bongo wenye majina makubwa kabisa lakini kazi zao ni kidogo au hazieleweki au hazilingani na uzito wa majina yao ktk jamii.
Kwa mawazo yangu nitalist watu wachache hapa!

1.WEMA SEPETU.
Kazi za huyu mdada nizujuavyo ni muigiza muvi na kumiliki kampuni na ni kazi ambazo si kuubwa kivile kulingana na jina lake.

2.STEVE NYERERE
jamaa alijichukulia umaarufu kwa kuigiza sauti ya mwl.jk na baadae akapindukia kwenye uemsii na movie acting...ofcoz kazi anazo zifanya ni nzuri lakini jina lake nikubwa saana ktk jamii kuliko hizo kazi.

3.MWIGULU NCHEMBA
jamaa ni naibu waziri wa fedha na nikiongozi ktk chama cha ccm.tofauti na wanasiasa wenzake huyu jamaa jina lake limevuma sana nakugeuka kua kubwa kiasi kwamba halilingani na kazi zake.

4.MAMA KANUMBA
huyu ni mama wa muigizaji maarufu marehem stv.kanumba....jina lake limeanza kutawala media karibu na kipindi cha mwisho mwanae yuko duniani lakini likavuma zaidi baada ya kifo cha mwanae.
Nisikiavyo kwa sasa anaigiza lakini ukweli ni kwamba pamoja na kazi hiyo ya uigizaji baado jina lake ni kuubwa sana kulingana na kazi yake.

5.HEMED PHD
jamaa ni muigizaji na mwnamuziki..alianza kujulikana kupitia tusker project fame na baada ya hapo umaarufu wake umepanuka kiasi kwamba nimkubwa kuliko kazi azifanyazo.

6.KIM KADASHIAN
ni demu wake kanye wizzle pia anashirik kwenye tv show ya familia yao.amekua na scandals nyingi lakin yenye umaarufu ni ile ya sex tape yake na ray jay.binafsi namuona ana jina kubwa kuliko kazi zake.

7.LUPITA NYONG'O
ni mkenya aliekulia mexico na kwa sasa anaishi marekani.amepata umaarufu baada ya kushiriki ktk movie ya 12years a slave na movie hiyo pekee imempa tuzo zaidi ya 25 ikiwemo ile maarufu ya oscar.na ni juzi tu ametokelezea kwenye mistar ya wimbo wa jayz(we made it).jinsi jina lake linavyo ng'aa si sawa na kazi zake zilivyo kwa sasa

8.DAVID MOYES
Jamaa ni kocha wa the red devils..jina lake limevuma sana baada ya kukabidhiwa timu na babu (sir) na baada ya hapo akaanza kuchezea kichapo mpaka na timu za mchangani.
Jina lake ni kubwa kuliko kazi yake.

.......na wewe tuwekee wa kwako hapa!
 
Umaarufu wa Moyes ulishakwepo kabla ya Man U labda we si mfuatiliaji wa mpira.
Sema tu anatajwa kwa sasa hivi kwa vile Man U ilikuwa timu tishio but baada ya kuingia man u kila siku wanatandikwa tu.

Mashabiki wa Man U wanasema "Kwanini Moyes hakuwa mojawapo kwenye ndege la Malysia iliyopotea!"
 

Ha ha ha ha....
Hapo kwenye ndege hapo mimi hoi!
Any way ni kweli mimi si mzuri kwenye mambo ya football lakini imefika hatua ili jina la "moyes" limenijaa kichwani sana japo kua nimesikia alikua maarufu!
Ila nionavyo mimi jina lake limekua kubwa kuliko kazi yake kwa sasa!
 
Na wengine umewasahau Kina Ustadhi Juma na Musoma,ndama mtoto wa ng’ombe,na Mzee Alex hao wana umaarufu sana hapa mjini ila kazi zao hazifahamiki

Zamani nilidhani labda wasanii wanarusha majina ya watu kwenye nyimbo kwa ajili ya ushikaji tu,ila hao sidhani kama ni ushikaji
 
Zamani nilidhani labda wasanii wanarusha majina ya watu kwenye nyimbo kwa ajili ya ushikaji tu,ila hao sidhani kama ni ushikaji

....nimestaajab nilipoona ktk baadhi ya threads humu jf kua hawa akina kiumbe na wenzie huwa wanamtindo wa kuwapumlia visogoni vijana wa kibongo fleva!
Swali likabaki kua kama vijana wana pumuliwa kisogoni,je vipi madada zetu?
 

ha ha ha h huyu jamaaa ni dodoki sana..mbulumundu mmoja hivi!
 
Nature abhors a vacuum.

Ukiona watu wasio na sifa kubwa wanatawala kujulikana, ujue wenye sifa hawajapatikana.

Ukiwa jangwani pasipo maji unaweza.kunywa hata maji machafu na kufurahia.

Kuna watu wanaona aibu Hollywood haitoi mwanamke mweusi (sio mix hawa kina Halle Berry) kuwa a big star, kwa hiyo wakiona anakuja mtu ana harufu tu ya kuwa star na kaenda Yale drama, anaweza kujieleza etc, watu wana jump at the chance kama kumchagua Obama waondoe lawama ya ubaguzi.

Lupita ame act vizuri, but her meme.is bigger than her acting. Nilivyosikia accolades nikafikiri she carried the movie kumbe hata sehemu aliyo act si kubwa hivyo. Not to be a hater or anything.

Na watu wengine wanapenda trivial intrigues, kwa hiyo kwao article ya Mama Theresa alivyosaidia yatima Calcutta inaweza kuwa boring, wakati article ya mpenzi mpya wa Wema inaweza kuwa inavutia.
 

...huwa nakuwa makini mtu kama kiranga akiandika..na kweli nimepata point hapa kwenye uandishi huu.
..me like this!
 
Na watu wengine wanapenda trivial intrigues, kwa hiyo kwao article ya Mama Theresa alivyosaidia yatima Calcutta inaweza kuwa boring, wakati article ya mpenzi mpya wa Wema inaweza kuwa inavutia.
Ila nadhani kuna wengine ni wanajua kuchukua attention ya watu,ndo maana hata akifanya kitu cha ajabu anajulikana zaidi kuliko anayefanya kitu cha maana.
 
Miaka ya nyuma ukisikia mwanamuziki anakubalika ujue kazi yake ndiyo iliyomfanya akubalike. Siku hizi kuna redio za watu ambazo hukuza watu tofauti na uwezo wao.

Kwa mantiki hiyo sishangai mtu kuwa na jina kubwa kuliko uwezo halisi
 
Ila nadhani kuna wengine ni wanajua kuchukua attention ya watu,ndo maana hata akifanya kitu cha ajabu anajulikana zaidi kuliko anayefanya kitu cha maana.

Attention ya watu inabidi tujiulize ya watu gani?

Kuna watu wakiona habari za Wema Sepetu na Kim Kardashian wanaruka, hawasomi.

Ila mara nyingi the hoi polloi outnumbers the highbrow and eggshells, kqa hiyo, kwa sababu habari ni biashara, wanaojua kuvutia kwa mambo ya mass appeal wanapata coverage regardless of the substance.

Nikiandika article ya "The Future of Tanzanian Foreign Policy and The Legacy of Mulungushi Club" kichwa cha article tu ni challenge kwa wengi, wangapi wanajua Mulungushi Club ni nini? Watu wengi wataruka.

Lakini Wema anakesha instagram huko, in.some.ways sio fair kusema anajulikana bure tu, anafanya kazi sana ku maintain kujulikana kwake.

Inakuwa kaman kujulikana ndiyo kazi yake.

Na inamsaidia kupata kipato.

Kuna.mama mmoja alikuwa anaanzisha a movie company, akataka Qema aqe kwenye movies zake. Mama kaambiwa Qema kukaa naye mezani tu kuongelea hiyo movie ni milioni tano zonatakiwa.

Sasa mfanyabiashara ya umaarufu kama huyu huwezi kusema anajulikana bure.

Sam Mangwana aliimba "kujulikana kuna mambo ewe Ananiaa"
 
Kweli
Mfano..lady gaga

A big psrt of it is challenging orthodoxy.

Lady Gaga kaikata nyama na kuifanya nguo. Borderline crazy but also outlandish.

Katika Tanzania ya leo ambayo wanawake wanashindana kusuka na style za nywele, Wema kaja tofauti na upara kama Buddhist Bhiku au anaenda kwenye chemo.

Anawapa challenge wanaofikiri ulimbwende hauwezi kuendana ns kipara kwa mwanamke wa Tanzania ya leo.

Not everybody can do that.
 
Miaka ya nyuma ukisikia mwanamuziki anakubalika ujue kazi yake ndiyo iliyomfanya akubalike. Siku hizi kuna redio za watu ambazo hukuza watu tofauti na uwezo wao.

Kwa mantiki hiyo sishangai mtu kuwa na jina kubwa kuliko uwezo halisi

"Walijigeuza mussa fimbo zao hazikugeuka nyoka wakajigeuza nuhu safina zao zikatoboka sasa wamejigeuza mungu mtu wanaamua nani leo atatoka"
 
"Kwa mfano mimi natumia internet kuingiza hela kashfa kwangu ni opportunity ya kuingiza hela"--Le Mutuz Le Big Show.

King kong iii
Nikua mimi sijaelewa hii quotation(ukilinganisha na mada hii) au nikua kuna mada nyingine unaizungumzia?....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…