Kuwa kichaa na kukosa akili ni vitu viwili tofauti kabisa, ni kama Dunia na Alfa Sentauri.
Neno sahihi lingepaswa kuwa kuvurugwa akili - ambapo kisayansi kila mwanadamu ana kiwango fulani cha tatizo hilo.
Pili, hata mtu akivurugwa akili, kuna dhima (functions) zingine za ubongo ambazo hazijaathirika, na zinafanya kazi kama kawaida.
Kompyuta inaweza kuharibika mfumo wa ndani wa viendeshi vyake (drives) lakini ikaendelea kufanya shughulizi zingine kama kawaida.
Si ajabu mtu anayeitwa kichaa anaweza kuzaa na kumtunza mwanae vizuri hata kuliko mtu mwenye kisomo bora cha malezi.