WATU WENYE ROHO MBAYA NDIO WANAOFANIKIWA MAMAISHANI.
Dunia imebeba watu wa kila aina,wachapa kazi ,waviviu,wanyonyaji,majizi ,wachawi nk.
Kuna makundi ya tabia mbali mbali, kuna wapole ,wenye roho mbaya,wakali,wasamalia,wenye roho nzuri nk.
Sasa basi hapa nawazungumzia watu wenye roho mbaya,wanavyoweza ku survive na kutusua kimaisha,
Cha kwanza hili kundi huwa na shauku ya kufika mbali kimafanikio, hivyo wanapokuwa katika utafutaji huwa hawana mzaha na kitu kinaitwa pesa,
Mnaweza mkafanya nae dili,halafu dili mfanikishe ujifanye unataka kumzima,
Ohoo!!! my friend utajuta, huwa hawakubari atahakikisha unampa chake,kivyovyote vile utampa tu,
huwa hawaachi nyuma hata shilingi
Hata katika familia/ukoo hawa watu huwa wanajulika,huwa hawaangalii wewe ni nani na unaukaribu nae vipi,huwa hawabebi watu wazembe hata kidogo, na huwa hawatoi misaada kizembe, eti unakuja unasema mimi ni mtoto wa mjomba wako,nimetokea kijijini nimekuja kukusalimia,huna la maana lolote mbona utarudi mwenyewe bila kuambiwa,
Hakuna kucheka na mtu ,huwa wanapenda sana kutumia Wathesalonike 3:10 Kwa wale wavivu hawatanielewa, Kwa watu wa namna hiyo ndugu wapenda kitonga(kupe ) huwa hawakanyaji, na hubakia na maneno ya lawama tu ,
Roho mbaya hupelekea kutochezewa,kudhurumiwa,mali zako kutochezewa,kupe kukaa mbali na wewe,hata majirani hukutambua na kutoleta mazoea ya kijinga,hata mtu akija kwako anakuja na hoja inayoeleweka na si vihoja vya kipambe,
ROHO MBAYA NI KINGA ZIDI YA WANYONYAJI
Husaidia kujiimalisha kiuchumi na kufikia malengo, hukufanya kuto kuingiza bajeti zinazoibuka zisizo na msingi, sio kidogo tu flani amekumbwa na shida, unazama mfukoni na kupangua mipango uliyoiandaa, na husadia kuto sumbuliwa hovyo
LENGO NI NINI?
Lengo ni kujichimbia mizizi kiuchumi,kama ni mti basi tungesema mti wenye mizizi mirefu kwenda chini,ambao hata kimbunga kikija si rahisi kuuangusha,
Hapo sasa ndio unaweza ukabadilika kidogo na kuwa na roho nzuri,Kwa sababu mizizi yako imejichimbia chini, hata watu wakining'inia kwenye matawi yako huta anguka, utaishi vizuri na uzee wako utaumaliza vizuri bila kuwa msumbufu au ombaomba
View attachment 1201404
"Ishiwa damu utapata wa kukuongeze, ukiishiwa pesa hutapata hata salamu"