Watu wenye ulemavu nao wakumbukwa katika katiba inayopendekezwa.

Watu wenye ulemavu nao wakumbukwa katika katiba inayopendekezwa.

Dragunov Sniper

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
2,795
Reaction score
9
Kwa kipindi kirefu watu wenye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kuwawezesha kupata haki ya mawasiliano IBARA YA 4(4), Katiba Inayopendekezwa imeainisha haki mahsusi za watu wenye ulemavu.

Baadhi ya haki hizo ni: haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na kulindwa dhidi ya vitendo vinavyoshusha utu wa mtu mwenye ulemavu. Vitendo hivyo ni pamoja na ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu.

Vile vile, Katiba Inayopendekezwa inaelekeza kwamba watu wenye ulemavu wana haki ya kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika nafasi za uwakilishi na shughuli za kijamii, kuwekewa miundombinu na mazingira yanayofaa yatakayomwezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri, kupata habari, kutumia lugha ya alama, alama mguso, maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwa, kupata ajira, kufanya kazi na kupata huduma bora za afya na uzazi salama. Kutambulika kwa kundi hili kikatiba ni fursa nzuri ya kuhakikisha kwamba taifa letu linaondokana na vitendo ambayo vina sura ya ukatili, ubaguzi na unyanyapaa, na badala yake kuwapa fursa ya kujiendeleza kisiasa, kiuchumi na kijamii.
 
kwa kipindi kirefu watu wenye ulemavu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali.

Pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kuwawezesha kupata haki ya mawasiliano ibara ya 4(4), katiba inayopendekezwa imeainisha haki mahsusi za watu wenye ulemavu.

Baadhi ya haki hizo ni: Haki ya kuheshimiwa, kutambuliwa na kulindwa dhidi ya vitendo vinavyoshusha utu wa mtu mwenye ulemavu. Vitendo hivyo ni pamoja na ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu.

Vile vile, katiba inayopendekezwa inaelekeza kwamba watu wenye ulemavu wana haki ya kupata elimu kwa kutumia vifaa maalum na kushiriki katika nafasi za uwakilishi na shughuli za kijamii, kuwekewa miundombinu na mazingira yanayofaa yatakayomwezesha kwenda anapotaka, kutumia vyombo vya usafiri, kupata habari, kutumia lugha ya alama, alama mguso, maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwa, kupata ajira, kufanya kazi na kupata huduma bora za afya na uzazi salama. Kutambulika kwa kundi hili kikatiba ni fursa nzuri ya kuhakikisha kwamba taifa letu linaondokana na vitendo ambayo vina sura ya ukatili, ubaguzi na unyanyapaa, na badala yake kuwapa fursa ya kujiendeleza kisiasa, kiuchumi na kijamii.

bora umenena manaake wengi wanalalamika kuhusu mauaji ya albino, eti kuwa serikali imewasahau.
Nadhani sasa kwa katiba hii inayopendekezwa, watu wenye ulemavu watakuwa wamepata haki zao za kikatiba.

Ushauri wangu ni kuendelea kuisoma katiba hiyo na kuielewa na kufanya maamuzi sahihi katika kuipigia kura hapo baadae.
 
Asante Katiba Inayopendekezwa, kweli ni katiba inayojali watu. Nashukuru sana kwankuainisha haki za watu wenye ulemavu. Watu hawa wamenyanyasika sana na kwa kipindi kirefu lakini Katiba hii imewakumbuka. Sasa kazi kwetu watu wenye ulemavu tuipigie kura ya ndiyo ili haki zenu ziendelee kulindwa.
 
Back
Top Bottom