balozi SDG 10
Member
- Apr 17, 2024
- 8
- 8
Wanaweza
Wanaweza walemavu, tubadili dhana zetu. Wanaweza tuwape nguvu, tusiwadharau katu
Kawapa mola werevu, tuwaache wathubutu.
Wanaweza kisiasa, kuongoza nchi yetu. Wanaweza kwa hamasa, tuwape dhamana zetu
Ni wakati wao sasa, nao kuongoza watu.
Wanaweza kielimu, tupo nao mavyuoni. Ulemavu siwagharimu, tukawaacha pembeni. Sote inatulazimu, mikono tushikaneni
Tusiwakatishe ndoto, kuwaficha majumbani. Tambua ngali mtoto, anaweza kitu gani. Kisha tuivuke mito, tumpeleke shuleni
Wanaweza si laana, hio dhana haifai
mapenzi yake rabana, mmoja asie rai. Huumba anavyoona, mja usiwakebehi.
Wanaweza michezoni,vifaa kiwapatia
Wasifika duniani, rekodi wamefikia
Wanashiriki mbioni, medali wajizolea
Wanaweza tusimame,watetezi wa elimu
Washairi tusikwame,na tutunge wafahamu
Wananchi tulalame,wataipata salamu