Chosen12
New Member
- Apr 26, 2023
- 1
- 1
Tanzania tuna watu mbalimbali waliojaliwa vipaji vya akili na ubunifu wa hali ya juu. Serikali haijaweka mpango wa kuwatafuta watu hawa na kuwatengenezea mazingira ya kuwaweka pamoja ili waunganishe mawazo na kuleta ubunifu wenye tija katika maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini.
Vitu vinavyosababisha ukosefu wa wabunifu wa nyenzo za sayansi na teknolojia
1. Kupuuza vipaji vya watoto wadogo.
Kuna baadhi ya watoto ambao wamejaliwa akili ya hali ya juu, serikali haina utaratibu maalumu wa kuwatengenezea mazingira mahususi kwa ajiri ya kuendeleza vipaji vyao, ili vije kutumika kubuni vitu mbalimbali vinavyokuza sayansi na teknolojia ya nchi yetu. Mfano video ifuatayo inamuonyesha mtoto mwenye akili isiyokuwa ya kawaida ya kuelezea baadhi ya vipengele vya mada za somo la fizikia kidato cha Kwanza ikiwa bado hajaanza shule.
Chanzo: Tbc online
View: https://www.facebook.com/simutv.tz/videos/1173895086070934/?mibextid=rS40aB7S9Ucbxw6v
Watoto kama hawa ni hazina kubwa kwa taifa letu serikali haioni umuhinu wa kuwatafuta na kuwajengea mazingira yanayowawezesha kukuza ubunifu kutokana na akili walizibarikiwa za hali ya juu ili baadae wabuni vitu mbali mbali kutokana na akili zao, badala yake jukumu hili wanaachiwa wazazi wao.
2. Serikali haizingatii vipaji na ubunifu wa watu walioko mtaani ambao hawakupata elimu rasmi ya shuleni.
Kuna watu wengi mtaani Wana akili ya kubuni nyenzo mbali mbali za kisayansi na teknolojia japokuwa hawakupata elimu ya juu, serikali haina mpango madhubuti wa kuwaendeleza watu hawa na kuwawekea mazingira ya kupanua wigo wa akili za ubunifu wao kwa ajiri ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ya nchi yetu ya Tanzania. Video ifuatayo inamuonyesha kijana ambae hajapata elimu ya juu lakini kaweza kutengeneza mfumo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji yanayotiririka mtoni.
Chanzo: Ayo tv
View: https://www.facebook.com/mapenziyoteonline/videos/691185704680920/?mibextid=rS40aB7S9Ucbxw6v
Vijana kama awa wanatakiwa kupewa kipaumbele kwenye bajeti za serikali zinazousu masuala ya sayansi na teknolojia, bila kuwatumia awa tunaweza kuchelewa kwenye maendeleo ya teknolojia.
3. Wanafunzi wenye akili ya hali ya juu wakipewa udhamini wa masomo nje ya nchi na kupata ufaulu wa hali ya juu huwa hawarudi nchini kuisaidia nchi yetu kuendeleza teknolojia kutokana na maarifa na ubunifu waliouiga nje ya nchi, badala yake wanafunzi hawa huchukuliwa na nchi za nje kwa ajiri ya manufaa yao binafsi, kwa namna hii teknolojia yetu haiwezi kukua kwa kasi pasipo kuwatumia wazawa waliopata maarifa kutoka nchi za wenzetu kuendeleza sayansi na teknolojia nchini Tanzania. Itakuwa hamna umuhimu wowote wa kupeleka vijana nje ya nchi kusoma Kisha wakabaki hukohuko kuzitumikia nchi za wenzetu ambazo teknolojia zao zishaendelea.
4. Wanafunzi wenye akili za hali ya juu na ujuzi unaothibitishwa na ufaulu mkubwa baada ya kumaliza masomo yao ya vyuo na vyuo vikuu serikali haijaweka mpango wa kuwakutanisha pamoja ili waunganishe mawazo na ujuzi wao katika kuunda vifaa mbalimbali vya kisayansi na teknolojia, badala yake watu hawa wanashindaniwa na makampuni binafsi ili yakawatumie katika ufanisi wa kazi zao. Watu hawa ni miongoni mwa nyenzo muhimu zinazotakiwa kutumika kama chanzo cha ukuaji wa sayansi na teknolojia nchini Tanzania.
5. Serikali inatengeneza taifa lenye idadi kubwa ya watu wenye elimu ya sanaa kulinganisha na elimu ya sayansi asilia. Ili teknolojia ikue kwa kasi inahitaji watu wenye maarifa ya elimu na ubunifu wa kisayansi, tukiwa na wanasayansi wachache tutachelewa sana kuendelea kwenye nyanja za sayansi na teknolojia.
Nini kifanyike ili tupate bunifu mbali mbali za kisayansi na kiteknolojia?
Gari Lina mifumo mingi ndani yake kama vile mfumo wa breki, mfumo wa injini, mfumo wa magrudumu manne nk. Kila mfumo una mgunduzi wake,kuna mtu aligundua mfumo wa breki, mtu mwingine akagundua mfumo wa umeme, na mwingine akagundua mfumo wa injini, baadae wakaunganisha mifumo hiyo na kutengeneza gari ambalo tunaliona hivi leo.
Hivyo basi ubunifu unahitaji muunganiko wa watu mbalimbali wenye fikra na mawazo tofauti tofauti ya kisayansi. Ni vyema serikali ikaweka mazingira yatakayoweza kuwakutanisha watu wenye bunifu mbali mbali na vipaji tofautitofauti ili waweze kupata urahisi wa kuunganisha vipaji vyao,mawazo na bunifu mbalimbali hapo ndipo teknolojia itakapoanza kukua kwa kasi, jambo hili linaweza kufanikishwa kwa njia zifuatazo :
1. Kuhakikisha angalau kila mkoa kuna kituo kimoja chenye uwezo wa kukutanisha watu wenye vipaji vya ubunifu kutoka katika mkoa huo bila kujali viwango vya elimu zao, vituo ivyo viwe na miundombinu na vifaa vyote vya muhimu kwa ajiri ya kuwawezesha kutanua ubunifu wao. Vituo ivi viwe na kituo kimoja kikuu katika kila kanda ya Tanzania ili kuweza kuwakutanisha wabunifu bora zaidi kutoka katika kila kituo kwenye mkoa. Kuwepo kituo kimoja cha kitaifa kinachowakutanisha wabunifu kutoka kila kituo cha Kanda ya Tanzania. Vituo hivi viwe na usimamizi imara na vitengewe bajeti ya kutosha kwa ajiri ya mafanikio makubwa ndani ya miaka kadhaa mbeleni.
2. Watoto wadogo wanaoonesha vipaji vya kuwa na akili isiyokuwa ya kawaida wawe na vituo vyao maalumu ambavyo vitakuwa na jukumu la kuwapa elimu rasmi na kuendeleza vipaji vyao. Vituo ivi viwe na miundo mbinu bora zinazoitajika kwa kila kipaji cha mtoto.
Gharama zote zinazohitajika katika vituo hivi zilipwe na serikali badala ya kuwaachia wazazi lengo likiwa ni kuwa miaka kadhaa mbeleni watatumika kuleta mabadiriko kwenye teknolojia ya nchi.
3. Serikali ihakikishe wanafunzi wanaopewa udhamini wa masomo kutoka nchi za nje wanarejea kulitumikia taifa katika maendeleo ya teknolojia kwa kutumia ujuzi maarifa na bunifu walizoziiga kutoka nje ya nchi.
4. Serikali iweke mkazo kujenga taifa lenye wasomi wenye elimu ya sayansi badala ya kuzalisha wasomi wenye elimu ya Sanaa kwa wingi ambao elimu yao haiwezi kuwafanya kuwa wabunifu katika nyanja za kiteknolojia.
Mwisho: Tusiweke mkazo kusema kwamba dunia inaenda kwa kasi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia bali tuweke jicho nyumbani, je teknolojia tuliyonayo sisi hapa Tanzania inaweza kutufanya tuwe na ujasiri wa kusema Tanzania inaenda kwa kasi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia? Kama hatuna huo ujasiri basi serikali ijitahidi kujikita zaidi kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia ili tuendane na ile kasi ya dunia.
Mwandishi: MSAJIDU ATWENDA FADHILI
simu: 0694450757
Watsap: 0763789850
Email: fadhilimsajidu@gmail.com

Upvote
2