Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Maendeleo yetu kama taifa yanategemea sana ni kiasi gani watu wetu wameelimika pasipo elimu hakuna maendeleo ya maana tutakayofanya.
Ili twende mbele kama taifa ni lazima tuwe na watu walioelimika. Ni lazima tuwe na watu wanaojua na sio wanaobahatisha, kila mtu katika nafasi yake na katika fani yake. Hasa kwenye masuala ya siasa hakuna masuala ya kubahatisha. Siasa ndio inayojenga kila kitu kama tukiwa na watu wanaobahatisha ni tabu. Maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa yanategemea umahiri, akili, maono, hekima na busara za viongozi. Jamii iliyopangiliwa vyema hutokana na viongozi bora na wenye hekima. Hutokana na viongozi wenye nidhamu. Mpangilio katika jamii hutokana na taswira ya viongozi katika akili zao. Viongozi wasio na nidhamu hawawezi kujenga jamii yenye nidhamu na mpagilio katika mambo yake. Hata miji yetu itakuwa hivyo hivyo kwasababu kwenye akili za viongozi wetu kumekosekana mpangilio bora na hili linafanya miji yetu pia kuwa ovyo na isiyo na mpangilio. Ili ujenge jamii yenye mpangilio lazima uwe na akili yenye mpangilio. Hii ni kazi ya akili inatoa kilichopo ndani yake kutoka ndani kwenda nje. Lakini pili ni lazima tulipende taifa hili kama tunataka kuendelea, kama hatulipendi hatutaweza kulitumikia. Ukweli ni kwamba hatulipendi tunavyopaswa kulipenda. Matendo yetu yanaonyesha hivyo.
Kama viongozi wetu wanalipenda taifa hili wangezingatia utawala wa sheria, wangelinda haki za watu bila unafiki.
Ni haki pekee inayotuunganisha sisi kama raia wa taifa hili. Nje ya haki hakuna taifa litakaloitwa Tanzania. Tabia ya kujali raia wenzako na kuwa tayari kutumikiana ingekuwepo. Juu ya yote kupendana kama raia wa taifa moja. Tabia ya kuibia taifa isingekuwepo kwa hakika moja ya sababu ya kuturudisha nyuma kama taifa ni wizi wa mali za umma. Wakati tunajaribu kwenda mbele tunarudishwa hatua nyingi nyuma. Kama pesa isipokusanywa huduma za jamii zitazorota na taifa halitofanya kazi ipasavyo. Ndio maana hatuendi mbele ipasavyo. Kila raia wa taifa hili lazima awe na hamu ya kuona taifa lake likienda mbele. Kama taifa hili likishindwa tumeshindwa sisi kwa ujumla. Nadhani ni wakati sasa kuwa wenye busara kama taifa. Tuanze na elimu ili tuweze kwenda mbele, ili watu wetu wajitambue kama taifa. Wajue ni nini malengo yetu kama taifa ili waweza kushiriki ujenzi wa taifa lao wakijitambua.
Ni jambo la muhimu na la msingi watu wetu kuelimika. Nidhamu, maadili na maarifa, lazima viende pamoja ili elimu ikamilike.
Tukiwa na daktari asiyekuwa na nidhamu na maadili, tutakuwa hatujafanya kazi yeyote kama taifa, vile vile kwa mkandarasi, mwalimu na wana sayansi, wajenzi na watengeneza fenicha wote hao watakuwa hawana faida kama elimu yetu haitoenda sambamba na nidhamu na maadili. Tunahitaji watu hawa wote wazalishe lakini watazalishaje wasipokuwa na nidhamu na maadili? Hawa wote ndio wanaofanya taifa hili. Taifa bora ni lile ambalo kila mtu anafanya kazi na hao ni sehemu ya taifa hili. Ni lazima tuwajibike kwa taifa hili bila kuwajibika hatutotoka tulipo. Ni lazima tushinde nafsi zetu dhidi ya ubinafsi hiyo ndio njia pekee kwa taifa hili kuendelea.
Kuna kukata tamaa kwa watu wetu dhidi ya taifa lao. Hawaoni baadae yao itakuwaje. Hakuna matumaini. Tunahitaji kuleta matumaini hayo mioyoni mwa watanzania. Tunahitaji kuirudisha imani yetu kwa Tanzania ambayo imeporomoka kwa kiasi kikubwa. Nchi imekuwa ya watu wabinafsi hakuna ushirikiano kama taifa wa kufanya kazi pamoja ili taifa hili liende mbele. Maslahi binafsi yameyazidi kete maslahi ya Taifa. Hatupaswi kuwa hivyo.
Ni muhimu kujenga maadili ya taifa hili upya kama tunataka kwenda mbele. Watu wetu watakuwa ni wenye manufaa tu pale watakapokuwa na maadili na nidhamu.Wakiwa hivyo taifa letu litapata faida.
Kwahiyo ni muhimu watu wetu kuwa na elimu, lakini elimu iliyotengenezwa pia kuwapa nidhamu na maadili. Ili waweze kuongoza tabia zao katika kazi yao, katika jamii na Taifa. Na mahusiano yao na jamii.
Watu wetu hawatoweza kushiriki katika siasa kama hawana nidhamu na maadili na siasa ikawa na manufaa. Hatutaweza kujenga jamii nzuri pasipo nidhamu na maadili. Ili tuendelee lazima tuzingatie hili.
Elimu ambayo itawafanya watu wetu wafikiri na wapende kutafuta maarifa na kuongeza ufahamu wao. Ufahamu huu ni muhimu sana kwa taifa letu, na ndio msingi wa jamii iliyopiga maendeleo na iliyo huru. Jamii yeyote ambayo haina maarifa, bado haijatoka kwenye ujinga haiko huru.
Ni muhimu sana hili jambo kuzingatiwa. Baadae ya taifa letu itategemea sana elimu ya watu wetu hasa vijana ambao taifa hili baadae litakabidhiwa kwao. Misingi hii hujengwa.
Taifa imara haliji kwa bahati mbaya, ni mipango, pamoja na juhudi zisizofifia za kutaka kuona taifa likipiga hatua moja kwenda nyingine. li watu wetu kujikomboa kutoka katika ujinga na umaskini. Maadui wetu wakubwa toka tunaopata uhuru.
Kwahiyo hii kazi ni kazi ambayo inahitaji umakini na nidhamu ya hali ya juu. Ni kazi ambayo inahitaji akili za watu wetu kuwekwa katika utaifa, na kuwa tayari kutumikia bila ubinafsi ili tutoke. Sio kazi ya mtu mmoja au wawili bali ni kazi ya umma.
Naangalia maendeleo ya nchi katika mtazamo wa maendeleo ya binadamu ya kiakili, na ndio maana nasisitiza kuwekeza katika elimu ili binadamu aendelee. Mitazamo ya watu wetu ikue, ili tuweze kujitawala na kuwa huru dhidi ya ujinga hili jambo linahitaji nidhamu. Nidhamu huleta mwelekeo.
Hatuwezi kupata ushindi dhidi ya ujinga kama watu wetu hawajaendelea kiakili au kama watu wachache wameelimika na wengine wameachwa nyuma katika maendeleo ya kiakili.
Kwasababu tunafamu katika mataifa yeyote yale, kuna tabia ambazo zinafanya mataifa kuendelea na kuna tabia ambazo hurudisha nyuma maendeleo ya nchi. Na ni jukumu letu kujenga tabia za watu wetu katika mwelekeo ambao utasaidia taifa hili kuendelea.
Kwahiyo ili taifa letu liendelee ni muhimu kuangalia tabia za watu wetu kwa ukaribu sana. Maendeleo kwa taifa hili ni kitu kinachowezekana, tuna kila kitu cha kutufanya tuendelee. Tuna watu ambao ni muhimu sana ili taifa lolote liendelee, na tuna ardhi ambayo tunatakiwa kuiendeleza na kuitawala. Maendeleo yeyote yale huletwa na watu kwahiyo ni wakati muafaka sasa kuwekeza kwa watu. Ni muhimu sana kuwekeza kwa watu maendeleo ya vitu ni matokeo ya kuwekeza katika watu. Kufanya mapinduzi katika akili za watu wetu na kujenga mitazamo yao upya.
Kwahiyo kama tunataka kuendelea lazima tujipange upya kila mtu katika nafasi yake na kulingana na kipawa chake na elimu yake. Tukijua kwamba sisi kama taifa tunatengeneza kitu kikubwa kinachofanya kazi kwa pamoja. Lakini ndani yake kuna vitu vitu vidogo vidogo vinavyotegemeana ili kitu kikubwa kifanye kazi. Kwahiyo tunahitaji viongozi ambao wataratibu watu wetu kila mtu katika nafasi yake, kusudi mfumo ufanye kazi vizuri na taifa lifanye kazi katika ufanisi. Binadamu tunategemeana sana, kuna madaktari, manesi, wanasheria, wahandisi na watu wengine wote lakini ili mfumo ufanye kazi vizuri lazima kuwepo na uratibu makini.
Naamini watu wote hawa ambao taifa limewasomesha makusudi yalikuwa ili taifa hili lisonge mbele na sio wapate manufaa binafsi bali manufaa makubwa ya umma. Sisi kama taifa ni kama mwili na viungo vyake kiungo kimoja kikiumwa mwili mzima unakuwa mgonjwa.
Kwahiyo ni muhimu sana kuunda mfumo utakaofanya kazi na kutoa faida. Katika taifa lililo kamilika lazima kuwe na watu wenye fani mbali mbali na kila mtu akifanya kazi katika ufanisi na katika uratibu mzuri. Hakuna taifa ambalo watu wake wanafanya kazi kibinafsi ambalo watu wake wanaweza kuonja maendeleo ni lazima wawe na dhamira ya maendeleo ya pamoja ili watoke. Hata kama kuna sekta binafsi lakini sekta binafsi lazima iundwe katika mfumo ambao baadae taifa litanufaika wakati huo huo watu binafsi wakinuifaika kwa kuweka maslahi ya taifa mbele.
Katika Taifa letu sasa kumetokea tabia ya watu kutaka au kugombea uongozi ambao hawana uwezo nao. Kuingilia fani ambayo kiasili ina watu wake, ambao wanajua undani wake. Sio kila mtu anaweza kuwa kiongozi. Pengine dhamira zao zinawatuma kufika pale kwasababu ya mali au umaarufu. Jambo hili ni hatari sana inahitaji busara kubwa kuwa kiongozi. Kwasababu maendeleo na baadae ya taifa lolote lile inategemea sana busara za viongozi katika kuamua mambo yatakayoamua majaliwa ya nchi.
Ikulu panahitaji akili iliyopevuka. Mamlaka na busara lazima viwe mikononi mwa mtu mmoja. Mtu akikosa busara akiwa na mamlaka ni hatari. Kwahiyo watu wanaotaka uongozi wa nchi hii lazima wajipime na kama waadilifu kweli waamue.
Tuna tatizo kubwa la nidhamu na maadili katika taifa letu. Jambo hili ni muhimu sana bila nidhamu taifa hili halitoweza kuendelea kuwa moja. Nidhamu katika kuongea kwetu na kuwajibika kwetu katika taifa. Uhuru wa kuongea na kutoa maoni sio uhuru wa kuongea chochote bila kutafakari madhara yake kwa jamii na kwa taifa. Kama unataka kuongea haswa mambo yanayohusu nchi kuwa mkweli na ongea kile ambacho una ufahamu nacho utakuwa umelifanyia kitu kikubwa sana taifa lako. Ama sivyo taifa hili litakuwa taifa lisilokuwa na dira. Tujifunze kusikilizana na kutafuta maarifa ambayo yatatusaidia.
Kila mmoja wetu ana jukumu la kumwelimisha mwingine katika jambo analolifahamu ili tujenge jamii yenye uelewa na yenye maarifa, kwahiyo ni muhimu sana kuangalia elimu na nidhamu za vijana na watoto wetu, kama tunataka taifa hili liwe na baadae njema. Tunapo tumia mitandao ya jamii tuitumie kama raia wanaowajibika kwa taifa lao. Tunapoongelea kuhusu uwajibikaji sio kwa viongozi tu hata kwetu sisi raia. Tuna wajibu kwa taifa hili na kila mmoja ana wajibu kwa mwenzake.
Sisi ni raia wa taifa hili tunaojiita huru, uhuru wetu unategemea sana tabia zetu na nidhamu zetu. Kwahiyo ni muhimu kutengeneza raia wanaojitambua na kuwajibika kwa taifa lao. Viongozi tunaowaona wanatoka kwetu na ni sehemu ya jamii yetu na wengine wengi watatoka miongoni mwetu kama hatujabadilika sisi, hakuna kitakacho badilika katika uongozi.
Kwahiyo tabia za watu ni muhimu sana maendeleo yetu yatategemea sana tabia zetu. Kuanzia ndani ya familia zetu, katika jamii zetu na katika taifa. Na mahusiano yetu pia yatategemea sana tabia zetu. Na bila mahusiano mazuri hakuna taifa tutakalojenga. Taifa hujengwa katika akili na mioyo ya watu na hubomolewa katika akili na mioyo ya watu. Tunatakiwa tuliweke hili katika akili zetu. Kwa sababu haya mambo ninayoongea ni ya msingi sana. Tutajidanganya kama tutafikiria maendeleo ya vitu pasipo kujenga mahusiano yetu kwanza. Mimi binafsi siwezi kuongelea kuhusu uchumi pasipo kuongelea mambo haya ya msingi kwanza, ambayo ndiyo yatakayo jenga amani ya nchi yetu na maendeleo ya kipindi kirefu. Kwahiyo ni muhimu raia wa nchi hii kutambua hilo na watu wanaotaka kugombea uongozi wa nchi hii.
Ni heshima kubwa kupewa nafasi ya kuongoza nchi na watu, na mtu yeyote mwenye akili ataheshimu hili na kutunza heshima yake. Kwa kuongoza watu kwa haki na uadilifu. Na si kinyume chake. Kuingia madarakani kwaajili ya faida binafsi ni ukengemfu.
Taifa kama taifa linahitaji dira na dira haitoweza kupatikana kwakuwa na viongozi mafisadi. Hatua ya kwanza kwa utawala wowote kuwa wa kikandamizaji ni pale watakapofikiri tu, kuanza kujilimbikizia mali. Hawatoweza kuongoza watu tena wata watawala kwa nguvu. Kiongozi hatakiwi kuwa hata na mawazo ya kujilimbikizia mali. Kuwa na mawazo hayo ni kumkaribisha ibilisi akutawale. Kwasababu hautojali haki wala maskini wa nchi.
Jambo jingine linalosumbua taifa letu ni kwa watu kutaka uongozi sababu ya sifa na umaarufu. Hili jambo ni la kijinga. Kiongozi anaongozwa na busara kufanya mambo yake na sio kutafuta sifa au jina wakati kichwani hamna kitu. Tafuta uongozi pale utakapokuwa na busara na hekima ya kutosha ya kuongoza watu.
Kwahiyo kiongozi wetu lazima awe mwenye kiasi katika mambo yake, mwenye busara na uwezo wa kusikiliza mambo na kuchambua, asiye jivuna yeye na familia yake. Mwenye uwezo wa kufanya maamuzi yenye hekima na anayestahili heshima katika jamii kutokana na mwenendo wake.
Jamii ambayo tunataka kuijenga ni jamii ambayo ina kiasi katika mambo yake, yenye nidhamu na inayoongozwa na fikra katika kuendesha mambo yake, lakini hatutofikia huko pasipo kuwa na elimu iliyobora.
Ndio maana nasema ni muhimu sana kuwekeza katika watu. Tukifikia hatua hiyo tutakuwa tumepiga hatua moja kubwa sana katika kuuondoa ujinga na kutengeneza raia wa nchi hii kuwa bora na wanaowajibika, ambao watasaidia taifa hili kuendelea.
Kwahiyo jambo la msingi ni watu, tunawajengaje ili wawe wenye manufaa kwa taifa? Hili ni swali la msingi la kujiuliza kama tunataka kuendelea. Tufanyaje ili watu wetu wawe na akili za utaifa?
Kwahiyo tunahitaji kurudisha mioyo ya watu na fikra za watu kwa taifa hili. Ni jambo la msingi na la kwanza. Tupate kujitambua kama sisi ni taifa tofauti na mengine.
Tuna ufahamu wetu na tunajitambua kama taifa. Na utandawazi hautotufanya kutojitambua sisi ni kina nani, kwa kuiga tabia na maadili ya nchi nyingine.
Ili taifa hili linyanyuke ni lazima likue kutoka ndani na kuelekea nje. Tukiruhusu ushawishi kutoka nje hatutaweza kukua na kuwa taifa linalojitambua na kujua nini lina kisimamia.Ni lazima tuwe na misingi kama taifa, taifa lisilo na misingi ni taifa lililo uchi.
Vijana wetu katika kuendesha mambo yao katika kila nyanja lazima wajitambue wao ni kina nani na wana wajibu gani katika taifa lao.
Wakipewa madaraka wajue wanawajibu kwa taifa hili na wamepewa heshima kutumikia na sio kufurahia mishahara minono wanayopewa na kusahau majukumu yao au kulewa sifa.
Taifa lazima liwaheshimu na kuwatunuku watu waliotumikia taifa hili kwa moyo mmoja bila ubinafsi. Haya mambo ni ya msingi sana katika ukuaji wetu kama taifa.
Malezi na makuzi ya watoto wetu ni msingi wa taifa imara la kesho. Tusipowalea vyema katika nidhamu tutakuwa na vijana wenye umri mkubwa lakini wenye akili ambazo hazijapevuka kushiriki katika masuala ya kijamii na wenye fikra ambazo si sahihi wasiojua baya na zuri kwa jamii na kwa taifa, na wasio na uwezo wa kupambanua mambo na kujadiliana vyema masuala yanayohusu taifa.
Kwahiyo muhimu kujiangalia kama taifa na kuona mwelekeo wa sasa sio. Ni matumaini yangu kwamba viongozi ambao wako madarakani huenda baadhi yao wanaliona hili. Kama wao hawalioni basi hawa wengine ambao wana mawazo ya kugombea uraisi wa nchi hii wanayaona haya niliyoyaandika.
Tunahitaji taifa letu kubadilika na kuwa lenye kufikiri zaidi na kufanya mambo kwa kufikiri. Tunahitaji kutoka hapa tulipo ili tujenge baadae nzuri kwaajili ya watoto wetu ili waje warithi taifa lenye utaratibu, maadili na nidhamu.
Taifa la namna hii linawezekana kabisa na amani ya kudumu itakuwepo kama misingi hii tutazingatia. Maendeleo ya mali yatakuja tu pale haya mambo mengine tutazingatia. Maendeleo ya kiakili ya watu wetu ni muhimu sana ni lazima tujenge tabia za watu wetu ambazo zitakuwa na faida kwa taifa.
Kujenga watu wetu kuwa waaminifu, waadilifu na wenye bidii katika kutafuta maarifa na katika kazi.
Nataka nikifa niache taifa hili watu wake ni wamoja na wenye kushirikiana. Na sio watu ambao wanaongozwa na mawazo ya ubinafsi. Hatuwezi kujenga taifa namna hiyo. Lazima tubadilike kama taifa.
Tuifufue elimu ambayo iliyosahauliwa kwa faida ya wote na watu wote tujihusishe katika kujielimisha sio kwasababu ya mshahara bali kwasababu ya ufahamu utakaotuongoza katika maisha yetu hapa duniani kama taifa na kuliosaidia taifa letu. Tujifunze kutumikiana na kuheshimiana. Hii itatusaidia sana kama taifa.