Ricky Blair
JF-Expert Member
- Mar 13, 2023
- 463
- 1,009
Nipo Ulaya; na kila ninachokiona na kunisikitisha ni jinsi watu weusi sisi tuna makelele sehemu zote na nyingi haswa tukiwa kw public transport au kw vyumba vya kushare; yaani lijitu linaongea masaa kw simu kwa nguvu zote kama roho inakata😡😡😡😡😡 na hajali Kama kuna watu wengine na ambao pia hawapendi( wazungu na watu weusi wengine kama mie) mtu una simu ya milioni unashindwa kununua earphones kweli??? Na hii tabia hata Bongo ipo kw daladala limtu linasikiliza mpira au movie kw loud speaker; jamani huu ni ushamba na mnatudhalilisha uku yaani wazungu wanaona waafrika wote wapo ivi; ukiwa unashare sehem na mtu usijiangalie wewe tu; ukiwa kw public transport, kw mgahawa au nini ukipokea simu nenda pembeni au sema kama sio dharura nipigie baadaye; sio kuongea kwa masaa na kwa sauti kama ya radi. Hii si sawa na tunawapa wabaguzi wa rangi silaha nyingine tu ya kutumia dhidi yetu. Mabadililo yanaanzia nyumbani. Hata kama chumba chako kichafu hata ukiwa ugenini hutosafisha chumba chako, ukiwa huoshi vyombo vyako baada ya kula pia ivyo ivyo. Tuanze kujirekebisha hii tabia naiona kutoka Bongo na huku waafrika kibao iwe kutoka Nigeria, Guinnea Bissau, Angola sijui wap hii tabia ipo. Ni tabia mbaya bwana si kila mtu anataka kusikia mambo yako. Kama unataka kuscream nunua ghorofa piga kelele lakini sio unashea sehem na mtu kisha unafanya huu upuuzi; alafu wakiambiwa ooh ubaguzi; umewahi kuona wazungu, wachina au wajapani wanafanya huu ujinga Bongo??? Mnatudhalilisha wengine uku mxieeeeeeu toleeni ushamba wenu uko Bongo kama walokole wenu wanapanda daladala kuubiri wakati kuna kanisa.