Mshangazi dot com
JF-Expert Member
- Nov 19, 2011
- 1,345
- 3,503
- Wanaotelekeza watoto wao na wanaokimbia majukumu ya kifamilia (ikiwemo kutunza wazazi wakizeeka).
- Wanaowaonea wivu wengine na kuweka nguvu kwenye kuwashusha kiuchumi na au kuwazibia fursa kwenye shughuli zao za kujiingizia kipato.
- Wanaochepuka kwenye mahusiano na kuleta magonjwa kwa wenza wao.
- Wanaoiba, wabinafsi na wala rushwa.
- Wanaoharibu maisha ya mabinti na vijana wadogo hasa wa shule kwa kuwadanganya na kuwaingiza kwenye mahusiano yasiofaa.
- Wanaotoa siri na madhaifu ya ndani ya wenza wao wa ndoa kwa marafiki au familia zao.
- Wanaopiga na kunyanyasa wenza wao kihisia, ukatili wa kimwili, kisaikolojia (ikiwemo kuwanyima unyumba) na kwa kutumia dini au mila.
- Wanaoficha ndoa zao au mahusiano yao ili kuwarubuni wengine.