nyeusi kulwa
New Member
- Nov 7, 2024
- 1
- 0
Zaidi ya watu elfu kumi waliokuwa wanategemea machimbo ya dhahabu katika eneo la Ifugandi, wilayani Nyang'wale mkoani Geita, wanadai kuathirika kutokana na zuio la shughuli zote za uchimbaji katika eneo hilo zuio hilo limesababisha maisha ya wengi kuwa magumu kwani wamekuwa wakitegemea uchimbaji wa dhahabu kama chanzo cha mapato yao ya kila siku.
Zabron Amesanga, mwenyekiti wa chama cha ushirika cha wachimbaji wadogo wa Ifugandi, amesema kuwa tayari wameshafika kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita ili kuomba muafaka juu ya mgogoro huu ambao umedumu kwa zaidi ya miezi sita. Ameeleza kuwa hali ni ngumu kwa wachimbaji wadogo ambao wameshindwa kuendelea na shughuli zao kutokana na zuio hilo.
Baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaonyesha wasiwasi juu ya baadhi ya viongozi, wakidai kuwa huenda ndio chanzo cha mgogoro huo na kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati ili kutafuta suluhu ya kudumu ambayo itawawezesha kuendelea na shughuli zao za uchimbaji.
Wananchi wameeleza kuwa wameathirika kwani wengi wao wamekuwa wakitegemea machimbo ya dhahabu kujipatia kipato cha kujikimu kim
aisha.