Watuhumiwa 11 wa makosa ya kimtandao wakamatwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA 11 MAKOSA YA KIMTANDAO

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na timu maalum ya kuzuia na kupambana na makosa ya mtandao limewakamata watuhumiwa 11 wa makosa ya kimtandao kufuatia ufuatiliaji mkali unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Timu hiyo Maalum

Katika hatua hiyo Jeshi la Polisi na timu hiyo, limemkamata Alex Magoti (26) Mkazi wa Tabora Mjini na wenzake nane kwa tuhuma za kumiliki luninga za mtandaoni na akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitumika kusambaza taarifa za uongo au uzushi kuhusu, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakuu wa Serikali.

Watuhuhumiwa hao wamekuwa wakiweka taarifa zao za uzushi, uongo na upotoshaji kwenye luninga za mtandaoni zinazotambulika kwa majina ya BSUN Online TV, GATTU Online TV, TAMUTAMU online TV, KILIMANJARO online TV na nyinginezo. Mfano wa taarifa hizo ni kama “Rais Samia akosoa vikali utawala wa Rais JPM, aanika ukatili aliofanya (haukubaliki hata kidogo)”IMEVUJA VIDEO, MBOWE APEWA SHAVU…!”, “DENI LA TAIFA LAIBUA MAZITO MWIGULU KUTUMBULIWA…!”, “GHAFLA MKE WA MAGUFULI AFA…!”, “ITAKUTOA MACHOZI UKWELI WOTE KIFO CHA MAGUFULI”

Pia
, Jeshi la Polisi limemkamata, Joseph Mzava (19) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Biachara Dar es Salaam (CBE), kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kufanikiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao kwa kutumia laini za simu zenye usajili usio na majina yake.

Jeshi la Polisi pia limemkamata LI NAIYONG (48) raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi, na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha Shilingi Milioni Mia mbili ishirini na moja laki moja sitini na tatu na mia sita (Tshs 221,163,600)

Mtuhumiwa huyo amekuwa akituma vifaa visivyo rasmi kuwaunganisha watu kwa simu kufanya mawasiliano nje ya nchi kinyume na sheria za mmlaka ya mawasiliano Tanzania.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo, vifaa hivyo ni:

Simu za mkononi 23

Laini za Simu 437 za makampuni mbalimbali ya huduma za simu
zenye usajili wa watu tofauti tofauti.

- Kompyuta Mpakato 6

- Sim Box 5

- Routers 3

Power Bank 1

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari na sheria zinazohusika kuepuka kuchapisha taarifa za uongo na zile zitakazo zua taharuki kwa umma, Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa mtu/watu wote watakao vunja sheria, kanuni na miongozo inayoelekeza matumizi sahihi ya mitandao.

imetolewa na
Muliro J. MULIRO - ACP

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam
 
Attachments

Hata hivyo wamechelewa sana kuwatia mbaroni hao vishoka wa habari.

Huu uhuni wa habari za uzushi na uzandiki hazijaanza leo, ni za muda kitambo sana.

Unakuta kichwa cha habari "kikuuubwa" na hakiendani na content, mpaka mimi nikawa nashangaa vyombo vya ufuatiliaji vinafanya kazi gani!

wahalifu wa kimtandao wamekuwa ni wengi sana sasa hivi pamoja na matapeli wa "tuma ile hela" bado tu wanaendelea!
 
Kwa hayo hata Kibatala hawezi kukomenti.

Heko Jeshi la polisi Kanda Maalum-Mtandao.

Tusubiri mahakama sasa. Tumeona na kusikia kuwa kuna vithibitisho 'evidence' ...isije tukaambiwa vilikuwa virtual.
 
Jeshi la Polisi pia limemkamata LI NAIYONG (48) raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi, na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha Shilingi Milioni Mia mbili ishirini na moja laki moja sitini na tatu na mia sita (Tshs 221,163,600)
Usalama wa Taifa na TCRA kazi kwenu maana hawa wachina hawaaminiki
 
Mwanangu Joseph Mzava, wewe ni nyoko! Miaka 19 tayari unaishi mjini kupitia jina la JK!!

Yaani mimi baba yako nilipokuwa na umri kama huo wa kwako, nilikuwa mjinga tu wa kuvizia vitoto vya shule, ili nipate uzoefu wa yale mambo yetu yale!!

Maana nilichelewa kweli kuanza. 🤔
 
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA 11 MAKOSA YA KIMTANDAO

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na timu maalum ya kuzuia na kupambana na makosa ya mtandao limewakamata watuhumiwa...
Hao wafungwe wanatumalizia bando zetu tu
 
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA 11 MAKOSA YA KIMTANDAO

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na timu maalum ya kuzuia na kupambana na makosa ya mtandao limewakamata watuhumiwa 11 wa makosa ya kimtandao kufuatia ufuatiliaji mkali unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na Timu hiyo Maalum

Katika hatua hiyo Jeshi la Polisi na timu hiyo, limemkamata Alex Magoti (26) Mkazi wa Tabora Mjini na wenzake nane kwa tuhuma za kumiliki luninga za mtandaoni na akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitumika kusambaza taarifa za uongo au uzushi kuhusu, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakuu wa Serikali.

Watuhuhumiwa hao wamekuwa wakiweka taarifa zao za uzushi, uongo na upotoshaji kwenye luninga za mtandaoni zinazotambulika kwa majina ya BSUN Online TV, GATTU Online TV, TAMUTAMU online TV, KILIMANJARO online TV na nyinginezo. Mfano wa taarifa hizo ni kama “Rais Samia akosoa vikali utawala wa Rais JPM, aanika ukatili aliofanya (haukubaliki hata kidogo)”IMEVUJA VIDEO, MBOWE APEWA SHAVU…!”, “DENI LA TAIFA LAIBUA MAZITO MWIGULU KUTUMBULIWA…!”, “GHAFLA MKE WA MAGUFULI AFA…!”, “ITAKUTOA MACHOZI UKWELI WOTE KIFO CHA MAGUFULI”

Pia
, Jeshi la Polisi limemkamata, Joseph Mzava (19) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Biachara Dar es Salaam (CBE), kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kufanikiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao kwa kutumia laini za simu zenye usajili usio na majina yake.

Jeshi la Polisi pia limemkamata LI NAIYONG (48) raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi, na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha Shilingi Milioni Mia mbili ishirini na moja laki moja sitini na tatu na mia sita (Tshs 221,163,600)

Mtuhumiwa huyo amekuwa akituma vifaa visivyo rasmi kuwaunganisha watu kwa simu kufanya mawasiliano nje ya nchi kinyume na sheria za mmlaka ya mawasiliano Tanzania.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo, vifaa hivyo ni:

Simu za mkononi 23

Laini za Simu 437 za makampuni mbalimbali ya huduma za simu
zenye usajili wa watu tofauti tofauti.

- Kompyuta Mpakato 6

- Sim Box 5

- Routers 3

Power Bank 1

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa rai kwa Wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, pamoja na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari na sheria zinazohusika kuepuka kuchapisha taarifa za uongo na zile zitakazo zua taharuki kwa umma, Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa mtu/watu wote watakao vunja sheria, kanuni na miongozo inayoelekeza matumizi sahihi ya mitandao.

imetolewa na
Muliro J. MULIRO - ACP

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam
Tanzania ni nchi yenye matundu mengi sana ukituliza akili vizuri unatoboa bila kudakwa hawa waliokamatwa michezo iliwakolea wakaona ndio kazi ya wao kuishi....
 
Back
Top Bottom