Watuhumiwa wa kifo cha Katibu wa Kanisa wafikishwa Mahakamani, ni Katekista na mwenzake

Watuhumiwa wa kifo cha Katibu wa Kanisa wafikishwa Mahakamani, ni Katekista na mwenzake

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Watuhumiwa wa mauaji ya mtumishi wa kanisa katoliki Makambako Nickson Myamba (46) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Njombe, Matilda Kayombo akitaja shauri namba 5 la mwaka 2022 linalowakabili Daniel Mwilango (42) na Nickson Nyamideko (23) kuwa ni la mauaji yaliyotokea Makambako mkoani Njombe.

Alisema marehemu alikuwa Katibu wa Halmashauri ya Walei Kanisa la Romani Katoliki Kigango cha Parokia ya Makambako mjini Njombe.

Alisema watuhumiwa hao wanadaiwa kuhusika na mauaji ya Nickson Myamba yaliyotokea Februari 7 mwaka huu huko mjini Makambako.

Wakili wa Serikali Magdalena Kisoka akisaidiwa na Paul Ngonyani walisema kosa wanalokabiliwa nalo ni Kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha kanuni ya adhabu Sura ya 16 ya sheria ya makosa ya jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Aidha, Hakimu Magdalena Kisoka amepanga tarehe ya kusikilizwa shauri hilo ambapo itakuwa tarehe 28 Februari 2022 kutokana na kutokamilika kwa upelelezi wa shauri hilo.

Hata hivyo watuhumiwa hao wamerejeshwa rumande kutokana na kesi inayowakabili kutokuwa na dhamana.

Watuhumiwa hao wawili Nickson Nyamwideko na Daniel Mwilango wanashikiliwa kwa tuhuma za kumpiga na chuma na kumkata kwa panga vipande vipande na kusababisha kifo cha Nickson Myamba kilichotokea mtaa wa Mangula Mjini Makambako mkoani Njombe.

Kuhusu mauaji hayo, soma:

FLyE8GCX0AIOumR.jpg

FLyE8nvXoAM0xgC.jpg
 
Pale Mbwa mwitu anapo jivisha ngozi ya kondoo! Sheria ifuate mkondo wake. Yaani Katekista mzima, unafanya tukio la kipuuzi kiasi hiki!
 
Sababu ya hayo mauaji ni nini?

Katekista alinyang'anywa tonge mdomoni! Yaani kiufupi kwenye ngazi ya ya chini kabisa ya Kanisa Katoliki (Kigango/Vigango), Makatekista huwa na nguvu na mamlaka, kiasi cha kujiona kama na wao ni Mapadre vile.

Na hiki ndicho kilichomkuta huyu Katekista. Baada ya kushtukiwa ni mbadhirifu, Paroko na waumini wengine wakaona isiwe tabu! Wakakubaliana kubadilisha utaratibu wa usimamizi wa duka la Kigango! (na hili ni jambo la kawaida sana), Katekista akamind! Na hivyo kuamua kutekeleza mauaji ya kikatili.

Thats why, nategemea sheria itafuata mkondo wake.
 
Mbona taarifa za awali zilisema mauaji yalitokea kanisani, leo inaandikwa mtaani, lipi la kweli na lipi siyo sahihi
Serikali za mitaa.

Ni eneo kubwa ambapo paweza kuwa na makanisa,shule nk. Hivyo hilo kanisa lipo kwenye mtaa wenye jina hilo labda
 
Mbona taarifa za awali zilisema mauaji yalitokea kanisani, leo inaandikwa mtaani, lipi la kweli na lipi siyo sahihi
Kanisa haliwezi kuwa mtaa huo?
 
hao jamaa wajinga sana,unaua mtu kwa mambo ya kuweza kupambana na ukayamilikk.
 
Katekista alinyang'anywa tonge mdomoni! Yaani kiufupi kwenye ngazi ya ya chini kabisa ya Kanisa Katoliki (Kigango/Vigango), Makatekista huwa na nguvu na mamlaka, kiasi cha kujiona kama na wao ni Mapadre vile.

Na hiki ndicho kilichomkuta huyu Katekista. Baada ya kushtukiwa ni mbadhirifu, Paroko na waumini wengine wakaona isiwe tabu! Wakakubaliana kubadilisha utaratibu wa usimamizi wa duka la Kigango! (na hili ni jambo la kawaida sana), Katekista akamind! Na hivyo kuamua kutekeleza mauaji ya kikatili.

Thats why, nategemea sheria itafuata mkondo wake.
Hatari sana kwa kweli
 
Back
Top Bottom