Watuhumiwa wa LBL wasiachiwe Huru, Mali zao zifilisiwe kuwalipa waathiriwa

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
Watumishi wa kampuni ya lbl wenye tuhuma za kuendesha kampuni kinyume na matakwa ya mfumo wasiachiwe huru. wananchi walioumia kwa tuhuma za kutapeliwa wahamasishwe kujitokeza kutoa ushahidi.

Ikibainika, mali na fedha za watumishi wa lbl zikamatwe na zifilisiwe ili wahanga walipwe stahiki zao. huku ndiko kuitendea haki katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania 1977 toleo 2005 ibara 26(1)(2), ibara 08(1) a,b,c, ibara 09 a,b,f, na h pamoja na ilani ya ccm 2020-2025 uk 01 ibara 04, uk 161-168, uk 08 ibara 10 na 11.

Niliisikia sauti yangu katika ulimwengu wa kiroho nikiwa ndotoni, nikawa nakoroma, sauti imenikauka baada ya moshi wa bangi kunivamia kutoka shamba lililokuwa likiungua huko porini. nikaanza kuropoka:

Tusome katiba ya ccm 1977 toleo 2022 uk 02 ibara 05(04), kisha tukasome kitabu cha binaadamu na maendeleo cha mwl. julius kambarage nyerere uk 17-21 kwa umuhimu wake, pamoja na mwongozo wa ccm 1981 uk 103-104 kwa msisitizo.

Tutumie neno kuufikisha ujumbe kwa walengwa.

Dkt Benson kalikawe bagonza, askofu mkuu wa dayosisi ya kkkt karagwe, nakumbuka tarehe 23/02/2025 alisema: neno lina nguvu sana, lina nguvu sana. mwisho wa kunukuu.

Wanaccm tumeapa kukataa fitna, ni lazima viapo vionekane katika matendo yetu ya kila siku ndani ya jamii ili kuonyesha tunayo nia ya kutenda haki kama tunavyotamka.

Tusome kitabu cha awamu ya tatu ya mradi wa kukiimarisha chama ukurasa wa 07 kwa msisitizo.

Balozi dkt emmanuel john nchimbi, katibu mkuu ccm taifa, akiwa katika harambee ya ujenzi wa ofisi ya ccm mkoa wa singida, nakumbuka tarehe 10/02/2025 alisema:

Tunasisitiza kuwa nafasi kubwa kuliko zote katika chama chetu ni kuwa mwanachama wa chama cha mapinduzi. ndiyo maana ni nafasi pekee katika chama chetu ambayo unaapishwa, hakuna nafasi nyingine yoyote katika ccm inayopata kiapo isipokuwa uanachama. mambo mengine yote yatatokana na katiba ambayo wanachama wameapa kuilinda. mwisho wa kunukuu.

Tusome katiba ya ccm 1977 toleo 2022 uk 01-02 ibara 05(02)(04)(05)(08)(09)(11)(16). tunapokula viapo, huwa kama tumeyavulia maji nguo, hivyo hatuna budi kuyaoga.

Kukiuka viapo vyetu ni usaliti kwa nchi.

Mheshimiwa rais dkt samia suluhu hassan, akiwa katika ufunguzi wa shule ya wasichana wilaya ya kilindi, nakumbuka tarehe 25/02/2025 alisema:

Wanasema waswahili, maji ukishayavulia nguo, ufanyeje? uyakoge. mwisho wa kunukuu.

Ilani ya ccm 2020 ibara 254 uk 303, ilani ya ccm 2015 uk 296 ibara 189 na 185(b), uk 303 ibara 255, uk 298-299 ibara 251(e), uk 04-05 ibara 07, ilani ya ccm 2015 uk 233-234 ibara 185(c).

mheshimiwa dkt sophia edward mjema, aliyewahi kuwa katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo ccm taifa, akiwa mkuu wa wilaya ya arusha, nakumbuka juni 2021 alisema:

tunachotaka ni kuhakikisha tunatatua na tunaelewa kero za wananchi wetu. tunataka saa zote tuwe tunawasikiliza wananchi. kazi yetu sisi ni kusikiliza saa zote na kwenda kutatua kero. mwisho wa kunukuu.

Tusome katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania 1977 toleo 2005 ibara 34(4) na 35(1) kwa umuhimu wake.

Tulipoinadi ilani kwa wananchi, tulitengeneza mkataba baina yetu na wananchi wa kutekeleza yote yaliyomo ndani ya ilani. kutoitekeleza ni kuvunja mkataba na kujipotezea uhalali wa kuaminiwa na wananchi.

Wananchi walioiweka serikali madarakani wametapeliwa. serikali ina wajibu wa kukomesha utapeli kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ibara 08(1) a, b, c.

Wananchi wamefurahi kukamatwa kwa matapeli lakini wanataka uwazi. wanataka hatua zichukuliwe dhidi ya vyombo vya habari vilivyoitangaza kampuni ya lbl na kuwafanya wananchi waiamini.

Wananchi wanahitaji haki zao, kwani watuhumiwa wako mikononi mwa polisi, ambao kimsingi hulinda raia na mali zao.

Mheshimiwa rais dkt samia suluhu hassan, katika ufunguzi wa shule huko handeni, nakumbuka tarehe 25/02/2025 alisema:

(viongozi) sikilizeni pande zote (zenye migogoro) na tupate uamuzi muafaka ili watu wajue wanaishi kwa amani. mwisho wa kunukuu.

Tusome katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania 1977 toleo 2005 ibara 12(1)(2) na ibara 13(1)(4)(5).

Nihitimishe kwa kurudia maneno haya:

Vyombo vyote vilivyohusika kuitangaza lbl na kuwafanya wananchi waiamini vilitenda makosa. vilikiuka sheria ya vyombo vya habari na sheria ya makosa ya mtandaoni ya 2015, hivyo kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ibara 26(1). lazima vyombo hivyo viwajibishwe.

Mheshimiwa rais dkt samia suluhu hassan, nakumbuka tarehe 23/02/2025 alisema:

Kaeni kitako, sheria zipo (zifuateni kwa ukamilifu wake), mmalize. maisha yaendelee. mwisho wa kunukuu.

Watumishi wa LBL wasiachiwe. watangazwe hadharani. wananchi wahamasishwe kujitokeza kutoa ushahidi.

Ikitathminika, wafilisiwe mali zao ili waliotapeliwa walipwe.

Huku ndiko kutendea haki viapo na kumfurahisha mungu tuliyemuapia kutenda haki.

Tuheshimu katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania, hasa ibara ya 08(1) a, b, c, ibara 26(1)(2), na ibara 09 a, b, f, na h.

Mheshimiwa pius msekwa, spika mstaafu wa bunge la tanzania, nakumbuka tarehe 21/02/2022 alisema:

Kila nchi ina katiba yake inayoiongoza. kila mwananchi anatakiwa kuiheshimu katiba na sheria zilizopo za nchi. ndiyo maana hata wabunge wanapokula kiapo, wanasema nitatekeleza masharti ya katiba iliyowekwa.

Tunapokula viapo, ni sehemu ya wajibu wa kila mwananchi wa nchi yeyote ile. kuheshimu katiba na sheria zote za nchi ni lazima.
mwisho wa kunukuu.

Viongozi na wananchi sote ni watu. kila mtu atimize wajibu na viapo vyake.

Nikashtuka ndotoni, kimya.

kidumu chama cha mapinduzi.

mathias mugerwa kahinga.
 
Wahanga wakutapeliwa na makampun uchwara mara nyingi ni walimu na police, ila walimu Huwa wanapaza sauti wakat Police wao Huwa wanauchuna kimya.
 
Wewe utakua mpya nchi hii. DECI mpaka leo hawajalipwa. Miaka zaidi ya 20
 
Back
Top Bottom