Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Leo July 12, 2024 imeitwa kesi ya Watuhumiwa tisa wa mauaji ya Mtoto Asimwe Novart aliyekuwa na ualbino ambaye alichukuliwa nyumbani kwao Kamachumu May 30 mwaka huu 2024 na June 17, 2024 mwili wake ulikutwa kwenye kalavati akiwa ameuawa na kukatwa baadhi ya viungo vyake.
Watuhumiwa hao tisa wamefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba kwa ajili ya kutajwa tena shtaka lao huku baadhi ya Watuhumiwa wakitokwa na machozi Mahakamani.
Wakili wa Serikali Erick Mabagala amesema bado wanaendelea na taratibu za kusajili shauri hilo katika Mahakama Kuu ambayo ndo ina Mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, Watuhumiwa hao wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia na uchunguzi wa shauri hilo no 17740 la mwaka 2024 tayari umekamilika.
Pia soma: Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji
Shauri hilo limeitwa tena mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba Elipokea Yona Wilson ambaye amesema Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote na wamerudishwa rumande mpaka July 26,2024 ambapo kesi yao itatajwa tena huku wakisubili kukamilishwa jalada lao.
Watuhumiwa hao tisa ni Elpidius Alfred Rwegoshora (49) ambaye ni Padri, Novat Venant (24) ambaye ni Baba wa Asimwe, Nurdin Ahmada, Ramadhan Selestine, Rwenyagira Alphonce, Dastan Buchard, Faswiu Athuman, Gozibert Arikad na Dezdery Everigist.
Miongoni mwa Watuhumiwa hao, Mshitakiwa namba moja ambaye ni Padri Elpidius Rwegoshora tayari ameweka Wakilk wa kumtete ambaye anaitwa Mathias Rweyemamu.