Watuhumiwa wa mauji ya Alphonce Mawazo waachiwa huru

Watuhumiwa wa mauji ya Alphonce Mawazo waachiwa huru

BabuFey

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2023
Posts
1,659
Reaction score
2,913
Radio Free Africa leo kwenye habari kwa ufupi saa nane mchana imeaarifu kuwa Watuhumiwa hao wame achiwa huru na mahakama baada mwendesha mashtaka kusema hana nia kuendelea na kesi.

Ikumbukwe marehemu alikuwa mchana mbele ya watu kwa mujibu wa taarifa za wakati huo.

Habari kamili kwenye taarifa habari usiku wa leo.

--
Mahakama Kuu Kanda ya Geita imewaachia huru washtakiwa wanne waliokuwa wakikabiliwa na shtaka la kumuua kwa kukusudia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.

Hukumu hiyo imetolewa juzi Juni 25, 2024 na Jaji wa Mahakama hiyo, Graffin Mwakapeje baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Washtakiwa katika kesi hiyo namba 56/2023 Alfan Apolnari, Epafra Zakaria, Hashim Sharifu na Kalulinda Bwire wameachiwa chini ya kifungu cha 91 cha makosa ya mwenendo wa jinai.

Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wakili Musa Mlawa akisaidiana na Deodatha Dotto aliieleza Mahakama kuwa chini ya kifungu cha 91, Jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kufuatia ombi hilo, Jaji Mwakapeje aliridhia na kuwaachia huru chini ya kifungu cha 91 na kueleza kuwa Jamhuri wanaweza kuwakamata tena watakapowahitaji.

Upande wa utetezi umeishukuru Mahakama kwa uamuzi huo kutokana na wateja wao kukaa ndani kwa miaka tisa tangu wakamatwe mwaka 2015 na kuishukuru Serikali kwa kuona haja ya kutenda haki.

Washtakiwa hao walitetewa na mawakili wa kujitegemea, Rukia Marandu, Siwale Siyambi, Costantine Ramadhan na Beatrice Amos.

Juni 18, 2024, kesi hiyo ilianza kusikilizwa upya baada ya Mahakama ya Rufani iliyoketi Mwanza mbele ya majaji watatu, Ferdinand Wambali, Issa Maigena Leila Mgonya kutengua hukumu ya kesi hiyo na kuamuru ianze kusikilizwa upya baada ya kubaini kasoro za kisheria katika mwenendo wa kesi hiyo Mahakama Kuu.

Mahakama ya Rufani katika hukumu hiyo, imesema imebaini mwenendo wa kesi hiyo ulikiuka masharti ya kifungu cha 246(2) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA).

Desemba 24, 2020, aliyekuwa Hakimu Mwandamizi Mkazi Geita, Frank Mahimbali, aliyepewa mamlaka ya ziada kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo iliyopaswa kusikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu, aliwahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne katika kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao walikata rufaa Mahakama ya Rufani wakipinga kutiwa hatiani na adhabu hiyo.

Mahakama ya rufani katika hukumu iliyotolewa Agosti 30, 2023 ilibaini kuwa kulikuwa na kasoro za kisheria katika hatua za kumpeleka mtuhumiwa mahakamani (Committal Proceedings).

Katika hatua hiyo, kwa mujibu wa kifungu 246(2) cha CPA, sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019, inataka idadi ya mashahidi watakaoitwa na Jamhuri watajwe pamoja na vielelezo vya ushahidi vitakavyotumika, visomwe kwa washtakiwa.

Hata hivyo, Mahakama ya Rufani ilibaini katika kesi hiyo baadhi ya mashahidi hawakuorodheshwa na Jamhuri na maelezo ya baadhi ya washtakiwa waliyoyatoa polisi hayakusomwa kwenye hatua hiyo lakini mashahidi walitoa ushahidi mahakamani.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma
 
Radio Free Africa leo kwenye habari kwa ufupi saa nane mchana imeaarifu kuwa Watuhumiwa hao wame achiwa huru na mahakama baada mwendesha mashtaka kusema hana nia kuendelea na kesi.
Ikumbukwe marehemu alikuwa mchana mbele ya watu kwa mujibu wa taarifa za wakati huo.
Habari kamili kwenye taarifa habari usiku wa leo
Haishangazi! Hili nililitegemea toka mwanzo. Damu ya Mawazo haitaenda bure!
Ilikuwa ni Mpango uliopangwa na kuratibiwa vizuri. Hakuna kinachoshangaza.
 
Mahakama kuu Kanda ya Geita imewaachia Huru watuhumiwa wanne waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauwaji ya Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Geita Alphonce Mawazo

Source: Mwananchi
 
Karma ndiyo ambayo itaamua hatma ya makosa yao. Binadamu anaweza kukutakasa kama vile apendavyo, lakini kamwe haitatokea mbele ya mamlaka ya mbinguni, haki yote ni lazima itendeke.
 
Mahakama kuu Kanda ya Geita imewaachia Huru watuhumiwa wanne waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauwaji ya Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Geita Alphonce Mawazo

Source: Mwananchi
Ilijulikana ilikua ni suala la muda tu!
 
Maisha haya! Daaaaah! Mama yake anataabika baada ya kuondokewa na mwanaye ambaye ndiyo alikuwa nguzo yake tegemewa kusongesha gurudumu la maisha.
 
CCM sijui kama kuna dhambi ambayo hawajawahi kufanya. Fikiria, kuna taarifa za uhakika kuwa mauaji ya Mawazo yalipangwa na kuratibiwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa, na mwenyekiti huyo hajawahi hata kuhojiwa. Ndiyo maana kule Mwanza watu waliona ni upuuzi kumkamata na kumpeleka Polisi mwenyekiti wa CCM mkoa aliyekuwa amemwua mtoto. Wananchi waliamua kumpa adhabu aliyostahili, wakamwua huko huko kwenye tukio.
 
Siasa za Afrika ni kitu hatari Sana kwa usalama wa Watu, hususani watu wale wenye fikra tofauti na fikra za watawala waliopo madarakani. Siasa ktk nchi zetu hizi za ki-Afrika ndio imekuwa chanzo kikuu kabisa Cha Mauaji ya Watu, mifarakano ya kijamii, chanzo Cha chuki kubwa iliyopindukia miongoni mwa watu, na pia imekuwa kiini Cha Maovu yote katika jamii za Watu wa bara hili la Afrika.
 
CCM sijui kama kuna dhambi ambayo hawajawahi kufanya. Fikiria, kuna taarifa za uhakika kuwa mauaji ya Mawazo yalipangwa na kuratibiwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa, na mwenyekiti huyo hajawahi hata kuhojiwa. Ndiyo maana kule Mwanza watu waliona ni upuuzi kumkamata na kumpeleka Polisi mwenyekiti wa CCM mkoa aliyekuwa amemwua mtoto. Wananchi waliamua kumpa adhabu aliyostahili, wakamwua huko huko kwenye tukio.
Kwani hawa wataishi jombaaa...acha watoke tu..Tunawangoja kitaaaa...bora hata wangebakia huko tu..wakala ngunga ya bure.....Tutawaibukia mashambani kwao mchana kweupeee..kama walivyofanya wao....mbona
 
Kazi inaanza sasa. Na hao waliohukumiwa kifo leo ni akina nani tena... Kweli huko mbinguni Tanzania itabaki kuwa kuwa channel ya vichekesho
 
Back
Top Bottom