Watuhumiwa wa Ubakaji Kuwakilishwa na wakili wa kujitegemea

Watuhumiwa wa Ubakaji Kuwakilishwa na wakili wa kujitegemea

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Leo ni siku ya tatu tangu watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wa binti wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam wafikishwe mahakamani na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Kesi hiyo itaendelea leo Agosti 21, 2024 kwa kuwasikiliza mashahidi ambao wameletwa na upande wa Jamhuri.

Kesi hiyo namba 23476 ya mwaka 2024 iliahirishwa jana kutokana na muda kuisha ambapo kati ya mashahidi watano walioletwa na Jamhuri walimsikiliza shahidi mmoja, ambaye hata hivyo hawakupata muda wa kumuhoji na wataendelea kusikiliza ushahidi wake leo.

Washtakiwa hao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea wakiongozwa na Godfrey Wasonga, Meshaki Ngamando, Boniventura Njeru na Sadick Omari Sadick huku upande wa Jamhuri kiwasilishwa na mawakili watatu.

Watuhumiwa hao wameshafika mahakamani kutokea ambapo kesi yao itaanza kusikilizwa muda

wowote kwenye chemba ya mahakama, ambapo watu wengine hawaruhusiwi kuingia isipokuwa mawakili na washtakiwa kutokana na unyeti wa kesi hiyo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Renatus Mkude amesema kinachoendelea kwa sasa ni kutoa ushahidi ambapo majina ya mashahidi yamefichwa ili kutoharibu wa kesi.

PIA SOMA
- Watu 4 wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani
 
Wapewe miaka yao mia tatu wakatulie huko mwanaume kwenda jela kwa kesi za Ubakaji ni ufala sana..
Kwa ushahidi upi? Kuthibitisha kosa la Kubaka kunataka ushahidi wa daktari. Je binti alienda kupimwa na daktari baada ya tendo? Au ndo alikimbilia kwenda kujiosha. Wakati mwingine inabid mtu umuelewe Theopista Tu.
 
Ushahidi wa Camera nadhani ni ushahidi usio na chenga ndio maana kesi za udharirishaji wanaweka TV kubwa kwenye hizo chamber court wakiangalia marudio ya mlichokifanya na watu wengi hawaruhusiwi kuingia fatilia hata hii itakua hivyo hivyo...
 
Video clip ilirekodiwa na Nani?
 
Wakili WA kujitegemea hulipwa dollar 75 Kwa Saa,,,200,000+tsh (serius crime).
 
Leo ni siku ya tatu tangu watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wa binti wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam wafikishwe mahakamani na kusomewa mashtaka yanayowakabili...
Nisichokielewa, kwanini kosa lifanyikie Dar halafu kesi ije kuungurumia Dom?

Naomba kueleweshwa hilo.
 
Hivi huyo wakili anayewatetea waliobaka anakuwa anatarajia kuwa atashinda kesi au ni kula pesa tu?
 
Wakili WA kujitegemea hulipwa dollar 75 Kwa Saa,,,200,000+tsh (serius crime).
mmh!hiyo dollar 75 ni kwa bongo hii au ulaya.? kumbe uwakili unalipa maana kuna kesi bongo hapa zinasikilizwa miaka!
 
Kwa ushahidi upi? Kuthibitisha kosa la Kubaka kunataka ushahidi wa daktari. Je binti alienda kupimwa na daktari baada ya tendo? Au ndo alikimbilia kwenda kujiosha. Wakati mwingine inabid mtu umuelewe Theopista Tu.
Don't tell me that where there's no doctor to examine a victim of rape, the offence of rape doesn't exist or cannot be proved.
 
Back
Top Bottom