BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Watumiaji wa simu za mkononi wameendelea kuongezeka nchini ikielezwa kuwa ni kutokana na mazingira wezeshi katika sekta ya mawasiliano kuelekea uchumi wa kijidali.
Hayo yamebainishwa katika ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyotolewa leo Oktoba 25 jijini hapa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna ongezeko la asilimia 3.4 ya laini za simu zinazotumika kufikia robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/23 kutoka laini 56.2 milioni Juni hadi laini 58.1 milioni Septemba.
Mikoa inayoongoza kuwa na idadi kubwa ya laini za simu zinazotumika hadi kufikia Septemba mwaka huu ni Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Tabora.
Ripoti hiyo inaonyesha pia licha ya ongezeko hilo hakuna kampuni yeyote ya simu ambayo ina zaidi ya asilimia 35 ya laini zilizosajiliwa.
Akizungumzia ripoti hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari amesema ongezeko hilo ni matokeo ya Serikali kuweka mazingira wezeshi katika sekta hiyo ambayo ni nyenzo muhimu kuelekea uchumi wa kijidali.
Amesema Katika kipindi hicho cha miezi mitatu watumiaji wa huduma za intaneti nao wameongezeka kwa asilimia 6.7 kutoka watu 29.1 milioni mwezi Juni hadi watu 31.1 Septemba.
Ameongeza kuwa, ongezeko la watumiaji wa intaneti limeongezeka kwa matumizi ya intanenti kutoka wastani wa MB 6,037 kwa mtumiaji Machi mwaka huu hadi MB 6,626 kwa mtumiaji kwa mwezi Septemba.