Watumishi 8 Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) wafunguliwa mashtaka 48

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826

Kupitia shauri la Uhujumu Uchumi namba 26/2023 lililofunguliwa Juni 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, ambapo washtakiwa waliokuwa waajiriwa TGFA, walisomewa mashtaka 48.

Mashtaka mengine waliyoshtakiwa nayo ni pamoja na Kuendesha Genge la Uhalifu, Kughushi, Kuchepusha, Kuwasilisha Nyaraka za Uongo, makosa ambayo yameisababishia Serikali hasara.

Washtakiwa walitakiwa kutojibu chochote Mahakamani na shauri limeahirishwa hadi Juni 27, 2023 litakaporejea kwaajili ya kutajwa tena.
 
kama hawaruhusuwi kujibu chochote unawapeleka mahakamani ya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…