A
Kama utaendelea kukaa kwenye utumishi niite mbwa, watakusaka.....Hapa hapa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala (MRRH), Watumishi wa Ajira Mpya hatujalipwa pesa za kujikimu, kila siku tunazungushwa.
Tusaidie sauti hii iwafikie wanaohusika.
Huyu Dogo watamterminate trust me 🤝 na wanavyokuwa waoga wakipigwa mkwara... Nafikiri ajiandae kisaikolojia kuanzia mada ilipo pandishwaUkitaka pesa ya wakati, jiajiri kijana.
Shukuru hata umepata kazi hiyo, wenzio wengi ulioshindana nao wamekosa kazi hiyo.
Nje ya mada: Kazi yeyote iwe ya serikali au binafsi, zinataka subra bwa mdogo, kuwa na nidhamu na ujifunze kutunza siri, kuwa na kifua kazini. Serikali ina milolongo mingi ya kulipa pesa hilo linafahamika, lakini pamoja na milolongo hiyo pesa waga zinalipwa japo sio kwa wakati. Kikubwa waga ni subra mahala pa kazi. Kazi ni kipimo cha utu, fanya kazi utalipwa fedha. Acha upumbavu huu wa kuja kuwaanika waajiri wako.