ZamdaIssa
JF-Expert Member
- Nov 10, 2015
- 879
- 1,458
Hongera mheshimiwa na Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutumbua majipu. Endelea na mwendo huohuo mpaka sisi wanyonge tupate walau kuonja keki ya Taifa hili japo kidogo!
Hongera pia Waziri Charles Kitwanga kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Usalama wetu uko mikononi mwako ingawa na sisi wenyewe wananchi tunajilinda.
Hon.Pres. Magufuli, Agizo lako kuhusu kubaini watumishi hewa linatekelezwa ijapokua kwa spidi ya Taratibu kidogo, Labda kutokana na ugumu wa kukusanya Takwimu(Sijui)
Mhe Rais, Tunaomba Umulike Jeshi letu la Polisi, watumishi hewa wako wengi, kila siku askari Polisi wa vitengo mbalimbali wanafukuzwa kazi, wengine wanaacha kwa ridhaa zao, wapo wanaofariki. Lakini cha ajabu salary slip za askari hawa bado zinatolewa kila mwezi kutoka Hazina! ina maana kwamba mshahara unaendelea kuingizwa kwenye account zao!
Nimesikia Watumishi wa Wizara hii wameshahakikiwa!lakini mheshimiwa Rais tunaomba Wizara irudie tena uhakiki huo kwa umakini zaidi, Wastaafu wengi wa Polisi wanapokea Mishahara isiyo halali!
Nina Imani Polisi peke yake inaweza kuwa na watumishi hewa zaidi ya 2000, Magufuli mulika!