A
Anonymous
Guest
Mimi ni mwalimu nimeajiriwa mwaka 2014.
Pamoja na kuwa ni mujibu wa sheria mtumishi kupanda daraja Kila baada ya miaka mitatu, sisi hatukupanda hata baada ya miaka 7, tulidhulumiwa madaraja mawili na serikali ya Magufuli, tukapewa daraja moja na mama mwaka 2021, Mungu amlinde Kwa Nia njema.
Nimeomba kwenda masomoni mwaka 2022 baada ya kutumikia daraja Kwa mwaka na nusu nikarubusiwa na mwajiri Kwa sharti la kujisomesha na nikakubali kusain mkataba wa ruhusa nikakabidhiwa barua.
Mwaka huu mwezi wa 6 wenzangu tuliopanda nao mwaka 2021 wamepanda madaraja, lakini mimi na wenzangu tulio masomoni tumeambiwa hatuna sifa ya kupanda kwasababu kuu 2, kwanza hatujajaza taarifa za utendaji kwenye mfumo wa PEPMIS, pili hatuwezi kupanda daraja ambalo hatujalitumikia!! Seriously! Mwaka 2017, tulitakiwa kupanda daraja tulilolitumikia na hatukupanda, mwaka 2020, tulitakiwa kupanda daraja linguine tulilolitumikia na hatukupanda, lakini leo tunaambiwa hatutapanda daraja ambalo hatujalitumikia.
Tunadhulumiwa, wanajua hatuna wa kututetea. Tukitoka shuleni tutapaswa kukaa tena miaka 3 ili tupande daraja hivyo tutakua tumepitwa madaraja mawili na tulioajiriwa nao na walioajiriwa mbele yetu.
Naamini siyo Nia ya mama Samia kutunyima haki zetu bali ni ujuaji wa baadhi ya watu wa utumishi. Swala hili litaathiri sana utendaji kazi wetu na madhara yake ni marefu.