nyanthorogo
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 220
- 402
Leo mke wangu ameenda kubadilisha kipandikizi katika kituo hiki Cha Afya Utegi, huduma hiyo ni ya bure, Cha ajabu wauguzi wakasema hawana vifaa mpaka atoe hela. Vifaa hivyo ni ganzi na kiwembe.
Wakamwambia anunue kachupa ka ganzi kwa sh 8,000/= Huku wakisemezama kana kwamba wanamsaidia kwa sababu kichupa kingemgharimu sh 12,000/=. Baada ya kuwapatia fedha ,vifaa hivyo vikapatikana hapo hapo hospital, Huku wakisemezama kuwa wateja wakiona gari limeingia wanajazana kutafuta huduma, wakiambiwa huduma hiyo haipo watoe hela hawaelewi.
Naomba uongozi wa kituo hiki Cha Afya Cha Utegi wawachunguze watoa huduma hiyo. Huu ni wizi wa mchana kweupe