KERO Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ni wababaishaji, hasa ofisi za RITA

KERO Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ni wababaishaji, hasa ofisi za RITA

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
Jul 20, 2024
Posts
42
Reaction score
98
Habari zenu,

Leo mimi kama member of JamiiForums nimekuwa na muda kupita ofisi za RITA halmashauri ya wilaya ya Kongwa, kiukweli nimesikitishwa na namna watumishi wake walivyo kosa weledi wa kujituma na kuwasaidia wananchi wake.

Hivi unakuta cheti cha kuzaliwa tu mtu unaambiwa njoo kesho na ili hali taarifa zako zote ziko sahihi, hawajui kuwa wananchi tunatumia gharama kubwa za usafiri kuja hapa ofisi za halmashauri, halafu kwa kirahisi mtu anakwqmbia njoo kesho. Je, ni kweli cheti cha kuzaliwa nachenyewe kimekuwa na michakato mingi kiasi kwamba kisiweze kukamilika ndani ya lisaa limoja, na sio kwamba kuna changamoto yoyote hapana isipokuwa wahudumu wengi wa hapa wanataka wananchi wawape vijisenti vya maji ili wawahudumie mbali na gharama tunazotoa za kupata cheti cha kuzaliwa ambazo ni 30,000.

Lakini bado wahudumu wanataka vijihela, yaani rushwa ndogo ndogo imeshamiri sana hapa ofisini. Kwa kukamilisha naomba RITA wafafanue hiyo elfu 30 inatumika kwenye nini, yani kupata cheti cha kuzaliwa kama haki ya raia wa Tanzania kuna ulazima gani sisi kulipa kiasi chote hicho na kinaenda kufanya kazi gani?

Pili, watumishi wa RITA ofisi za halmashauri ya wilaya ya Kongwa nini shida mpaka muwasumbue wananchi kwa kuwapiga kalenda kama vile mahakama ilihali mtu taarifa zake zipo sahihi ebu fikiri mtu anatoka mbali huko gharama za usafiri anatumia hata elfu 20 kwenda na bado hajarudi na bado aambiwa aje kesho na wakati mwingine maskini huyu anakuja hata awamu nne na bila kupata huduma.

Tatu, ofisi za NIDA kumekuwa na changamoto ya mtandao, yaani unakuta mwananchi akuja hapa ofisi za NIDA wilaya ya Kongwa karibia mara 3 mara 4, mtu huyo bado hajala, hivyo basi kwanini wizara husika au mamlaka ya NIDA iwafungie minara ikiwezekana mezani kwao kabisa ili wananchi wasipate adha ya kuja mara nyingi hapa wilayani.

Jamani serikali ilitizame kwa jicho pana suala hili wananchi tunaumia sana na huu usumbufu na wakati huo huo gharama za usafiri zikiwa juu.

Naomba kuwasilisha wakuu🙏🙏🙏🙏
 
hapa wanataka wananchi wawape vijisenti vya maji ili wawahudumie mbali na gharama tunazotoa za kupata cheti cha kuzaliwa ambazo ni 30,000.
Usichokijua hata kwenye hio 30k unakua umepigwa 10k gharama halisi ni 20k kwa mtoto miaka 10 na kuendelea 10 kushuka ni 7k. Na maxmum lead time ya kungoja cheti ni 1 week
 
Na hao watumishi.walishindwa tu kukwambia.kuwa maombi ya cheti cha kuzaliwa kwa sasa ni online pale ofisi za Rita utaenda kukichukua tu baada ya kufanya maombi mtandaoni wewe mwenyewe unaweza kufanya hayo maombi ndani ya dakika 15 tu.

Kila siku nasema WELEDI umepungua sana ofisi za umma
 
Back
Top Bottom