KERO Watumishi wa hospitali ya liwale iliyopo Liwale-Lindi walioajiriwa kwa mkataba na Halmashauri kupitia mdau MSF hawana tarehe maalumu ya mshahara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna watumishi wapatao 43 ambao wameajiriwa kwa mkataba Halmashauri ya Liwale kupitia mdau Medicines San Frontiers (MSF) au Madaktari wasio na mipaka miongoni mwao ni Madaktari, wauguzi na wataalamu wa maabara na wahudumu wa afya ngazi ya jamii zaidi ya 10.

Cha ajabu ni kuwa hawajapata mshahara wa mwezi Mei Hadi Leo na hawajui lini watapewa, Maana salary ya mwezi April ilitolewa tarehe 18/5/2024

Na hii imekuwa ni kawaida yaani hakuna tarehe maalumu ya mshahara.

Pia bima zao za afya hazifanyi kazi ni mwaka wa pili sasa.

Vilevile hawana access ya kuangalia mafao Yao yaani hawajui kama Hela zao za PSSSF zinafika sehemu husika au vinginevyo.

Lakini kibaya zaidi ni kuwa waliambiwa watapewa kipaumbe kwenye ajira za serikali.

Hilo halifanyiki kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…