Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
Wote wamepewa fedha sawa kwa darasa moja (Mil 20). Ninavyosikia (Sina uhakika), vifaa vya ujenzi (Nondo, bati, Cement) DSM ni nafuu zaidi kulinganisha na mahali kama Bukombe kutokana na umbali kutoka viwandani. Lakini nikiangalia viwango vya madarasa katika picha hapa chini inaonesha kabisa madarasa na madawati ya DSM yapo chini ya kiwango kuliko yale ya Bukombe.
Rais ulisema utawapima Wateule wako kutokana na kazi zao, nadhani chujio lako la kwanza kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi wao litokane na jinsi gani wamesimamia ipasavyo ujenzi wa madarasa haya. Hilo litakuwa ni fundisho kubwa sana kwao and next time wakitakiwa kusimamia mradi wowote hawataleta utoto utoto.
Hongereni sana Bukombe na Mkuu wenu wa Mkoa kwa kazi nzuri.
"Wahuni" aliosema Polepole ndio hawa wa Kigamboni, wanatakiwa wamalizwe sasa.
Madarasa ya Kigamboni (DSM)
Madarasa ya Bukombe (Geita)