Watumishi wa Serikali wa Kigalatia wanasali mara tatu kila siku, Mungu awasaidie waache Rushwa!

Watumishi wa Serikali wa Kigalatia wanasali mara tatu kila siku, Mungu awasaidie waache Rushwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Nimeshuhudia pale KKKT Azania Front na Anglican church St Albans Jumatatu hadi Ijumaa Watumishi wa Serikal wanajaza Kanisa Asubuhi, Mchana na Jioni.

Hali hii nilizoea kuiona kwa wale Islam wanaoswali Swala 5 lakini sasa Wakristo ndio wanaongoza kwenda Ibadani

Hasa Wagalatia wa TRA, RITA na Uhamiaji wanakuwa wengi sana Azania Front hasa Asubuhi na Mchana.

Sijaelewa kama ni kumtafuta Mungu wa mbinguni tu au ni Toba baada ya kila dhambi ama kurogana na roho mbaya ndio zimeota mizizi serikini.

Mimi nawatia Moyo Wapendwa Utafuteni kwanza Ufalme wa mbinguni na mengine yote mtazidishiwa, amen!
 
Hawaaminiki, usije ukawaiga, tazama zamani hawakuwa na jumuiya za kila Jumamosi, walikuwa wanawaponda wakatoliki hivi sasa nao wanajumuiya za kila Jumamosi na ndiyo majukwaa ya kuwagawa waumini wasiokuwa nacho na wale wenye nacho

Zamani hawakuwa wanasali mara kadhaa kwa siku, hivi sasa ndiyo hao!

Zamani walikuwa wanapata viongozi kwa neema ya Mungu, hapakuwepo kugombania madaraka, lakini leo hii, wanakwenda mpaka kwa waganga wa kienyeji kufanya mazindiko, wanasali na kufanya ibada za mazishi chini ya mitutu ya bunduki.

Mungu nifundishe kunyamaza juu ya wenzangu hawa.
 
Back
Top Bottom