A
Anonymous
Guest
Habari JamiiForums, nimekuwa mdau wa muda mrefu lakini pia nimekuwa napata malalamiko mengi sana kutoka kwa rafiki yangu mmoja hivi naomba langu lisitajwe.
Watumishi wa shule ya St Marys Secondary Mbezi wanaishi katika mazingira Magumu sana, watumishi hao wote hawana mikataba ya kazi. Huyu mtu wangu wa karibu tangu aajiriwe pale hana mkataba hadi alipoondoka pale alikosa stahiki zaje zote na hivyo kukosa base ya kuanzia maisha baada ya kutoka pale.
Utaratibu haujulikani ni upi unafukuzwa kazi tuu kama ulivyokuja na unaondoka hujui haki zako za msingi, kiukweli hii inaumiza, mamlaka husika zifanyie suala hilo kazi.
Mtu kafanya kazi miaka mitano unamfukuza bila utaratibu wowote bila kosa, mishahara hailipwi kwa wakati na mingi wanadai mfano mshahara wa mwezi wa 10, 11, 12, 01 katika hiyo miezi wamelipwa miezi miwili tuu haijulikani ni mwezi gani NSSF zao hazijulikani makato yao yapoje
Barua za ajira hawana
Barua za mikataba ya kazi hakuna
Wapo wapo tu.
Naomba kupaza sauti watumishi hao wasaidiwe.