Watumishi wa Umma 586,000 wametwishwa mzigo wa kuhudumia Watanzania zaidi ya milioni 65. Kwanini serikali haiwalipi mishahara mizuri?

Na posho ni kiasi gani watumishi wamezila hapo zikiweka wazi tunaweza tusiamini macho yetu.
 
Nimegundua watumishinwa umma ukitoa walimu na wanausalama, pamoja na kadre ya menejimenti, waliobaki ni songambele tu. Wanasubiri kupewa kazi na kufanya na wakishamaliza hawana jipya. Wengi ni data entry tu. Na serikali kwa kutambua hawa watu ni changamoto, ikawawekea mfumo.wa PEPMIS (Hope niko sahihi) kuhakikisha inawabana wawajibike ila bado wanalialia tu.

Ukimsikiza Rais hapo juzi wakati akipokea magawio toka mashirika ya serikali utagundua hawa watu ni viwavi. Wanapaswa kuzalisha na kujiendesha ila bado wanatega wapate ruzuku ya serikali. Yani sekta binafsi inakamuliwa kwenda kulipa watumishi wa umma. Nilidhani waliopaswa kufikiriwa kwenye nyongeza ni wafanyakazi toka sekta binafsi ambayo hata Rais aliisifia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…