Watumishi wa Umma kuna la kujifunza hapa!

Econometrician

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2013
Posts
16,879
Reaction score
31,253
Ni kwamba katika utawala wa Magufuli mwaka 2018/2019 baadhi ya Watumishi kwenye Taasisi ambazo zina majina walifanyiwa uchunguzi wa kimya kimya kwenye Akounti zao za mabenki.

Nasikia kuna mzee moja alikuwa anafanya kazi MSD, wakamkuta bank na fedha kiasi cha shilingi Bilioni 2 za Kitanzania, wanasema PCCB na jeshi la polisi walimsakama sana Jamaa.

Badaye jamaa alitoa vielelezo vyote kwamba hizo hela alikuwa nafanya saving kutoka kwenye mshahara wake pamoja na posho ambazo alikuwa anazipata Ofisini kwake toka alipo pata ajira yake ndipo wakamuachia.

Hili ni somo kubwa sana kufanya saving mpaka kupata 2B najua imechukua zaidi ya miaka 20 but huyu hata kuwa kama wastafu wengine ataenjoy maisha yake hadi siku anaingia kaburini.

Watumishi haya mambo yanawezekana, penye nia kuna njia.
 
Mkuu ulisemalo ni kweli, watu huwa tunahisi hatuna cha kusave lakini kiuhalisia ukiweka mipango utashangaa baada ya muda kuwa kuna hela nyingi zilipita mikononi mwako bila kufanya lolote la maana '' kama hakuna mipango, hakuna la kutimizwa''
 
Sawa inawezekana ila inategemea na familia unayotoka.Kama sisi kapuku wakijua una kazi tu basi shangazi,mjomba,ba mkubwa kifupi ndugu wote wataanza kukutolea macho wewe na unakuta hakuna namna lnabidi kusaidia familia.
 
Mshahara wa mtumishi wa umma kufanya saving hadi kufikia 2B kwa kipindi cha miaka lets say 30 unahitaji kuweka zaid ya 5.5M kila mwezi bila kukosa.
Naweka hesabu sawa tu hapa
 
Kwenye maisha ya utumishi wa umma huwezi kufanya maendeleo Kama utaogopa madeni uko benki kwaio Ni swala ambalo halikwepeki hasa kwa watumishi wa vipato vya kati.sema Ni muhimu kuzichanga karata vizuri ili usije ujaichukia kazi baada ya kuchukua huo mkopo
 
Mshahara wa mtumishi wa umma kufanya saving hadi kufikia 2B kwa kipindi cha miaka lets say 30 unahitaji kuweka zaid ya 5.5M kila mwezi bila kukosa.
Naweka hesabu sawa tu hapa
... Ajabu kweli. Savings ya 2B kwa miaka 20 aliyosema jamaa ni saving ya 8.4 m/= kila mwezi bila kukosa. Labda huyo ni wale waliokuwa wanalipwa 40 m/= kila mwezi sio watumishi wa umma tunaowajua!
 
Yaani ni vitu ambavyo haviwezekan ndomaana hii stori siwezi kuelewa kwamba na PCCB wamuachie tu kirahisi eti unasevu.

Bilion 2 ni lazima uwe na chanzo kingine au hizo hela aliziwekeza sio alisevu tu

Miaka 30 huyo alianza kazi enzi za mshahara sh 800 huko kasevu vipi mpaka awe na bil2
 
... Ajabu kweli. Savings ya 2B kwa miaka 20 aliyosema jamaa ni saving ya 8.4 m/= kila mwezi bila kukosa. Labda huyo ni wale waliokuwa wanalipwa 40 m/= kila mwezi sio watumishi wa umma tunaowajua!
Halafu mishahara ya Miaka 20 iliyopita sio kama ya sasa

Washua walianza na mishahara ya sh 2000 kwa mwez miaka hiyo pesa inashuka thamani eti mpaka saiv afikishe bil2 hesabu hazikubali hata kidogo

Au imagine kama unavyosema alisevu mil40 kwa mwezi. Hiyo mil40 alikua analipwa na nani mwaka 2000 au 1999 huko?? Hela nyingi sana hiyo kipindi hicho achilia mbali sasahivi.

Maelezo hapo ni haya
1.Aliiba
2.Aliwekeza huo mshahara
3. 1&2 kwa pamoja
 
Ni kwamba katika utawala wa Magufuli mwaka 2018/2019 baadhi ya Watumishi kwenye Taasisi ambazo zina majina walifanyiwa uchunguzi wa kimya kimya kwenye Akounti zao za mabenki.

Nasikia kuna mzee moja alikuwa anafanya kazi MSD, wakamkuta bank na fedha kiasi cha shilingi Bilioni 2 za Kitanzania, wanasema PCCB na jeshi la polisi walimsakama sana Jamaa.

Badaye jamaa alitoa vielelezo vyote kwamba hizo hela alikuwa nafanya saving kutoka kwenye mshahara wake pamoja na posho ambazo alikuwa anazipata Ofisini kwake toka alipo pata ajira yake ndipo wakamuachia.

Hili ni somo kubwa sana kufanya saving mpaka kupata 2B najua imechukua zaidi ya miaka 20 but huyu hata kuwa kama wastafu wengine ataenjoy maisha yake hadi siku anaingia kaburini.

Watumishi haya mambo yanawezekana, penye nia kuna njia.
Inategemea mambo mengi
 
Story hizo za kijiwen yule kenge akute bilioni mbili aziache
 
Back
Top Bottom