Watumishi wa Umma mliopata uhamisho Mei, Juni na Julai 2021 mmepokea barua zenu za uhamisho?

Watumishi wa Umma mliopata uhamisho Mei, Juni na Julai 2021 mmepokea barua zenu za uhamisho?

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
2,016
Reaction score
1,946
Kwa wale Watumishi wa Umma ambao wamebahatika kupata uhamisho unaotolewa na Tamisemi kati ya mwezi May hadi July 2021, vip kuna ambao wamepata vibali au barua za kuruhusiwa kwenda waliko hamia?

Mwenye taarifa zaidi tafadhali atujuze. Hii ni kwa sababu hali hii haijazoeleka kwa miaka ya nyuma kwani majina yalipo kuwa yanatangazwa kwenye tovuti ya Tamisemi basi barua zilikuwa zimeshatangulia kwenye halmashauri husika, lakini kipindi hiki jambo hili limekuwa tofauti sana maana mpaka sasa hivi bado barua hazijatoka.

Mwenye taarifa zaidi atushirikishe.
 
Inavyoonekana ni kuwa barua hazijatoka, ila hata mimi sielewi ni kwa nini. Tuliaminishwa na mh.Rais Kuwa Ummy Mwalimu (waziri wa TAMISEMI) na Prof. Riziki Shemdoe (Katibu mkuu wa TAMISEMI) wataupiga mwingi hapo wizarani.Lakini kwa mambo yanavyokwenda naona hakuna matumaini.
 
Kwani nini shida na je ni wote wale wa kuanzia mwezi mei? Maana Nina ndugu yangu kaona kina hii julai ila mpaka Leo hamna kitu wala hapati barua
 
Kwani nini shida na je ni wote wale wa kuanzia mwezi mei? Maana Nina ndugu yangu kaona kina hii julai ila mpaka Leo hamna kitu wala hapati barua
Hapo ndo kuna kitendawili, uhamisho wametoa tunashukuru, ila barua hazitoki ..sijui shida iko wapi...hii ni tofauti sana na miaka iliyopita
 
Kusema kweli hii inaathili utendaji kazi mfano ndugu yangu kanyimwa barua na mkurugenzi kisa hajaona barua za kuomba uhamisho kwnye faili akaamini alimruka na hivyo kakataa kutoa barua ambayo imetoka tanisemi sjajua kama Yuko sawa na Nini ashauriwe ndugu yetu
 
Back
Top Bottom