Kipindi cha Nyerere, maadui wa nchi walikuwa watatu: ujinga, magonjwa, na umaskini.
Ingawa hao maadui wangalipo, lakini huenda kuna adui mwingine kaongezeka: watumishi wa umma.
Mbaya zaidi ni kuwa huyo adui anaishi kwa jasho la wenye nchi kwa manufaa yake mwenyewe huku wenye nchi wakiumia.
Hapo chini ni clip ya mwananchi aliyezungushwa kwa miaka minne kupatiwa mchoro wa nyumba yake.
Fikiri, amelipa fedha zilizohitajika lakini bado alizungushwa miaka yote hiyo. Kama asingekutana na Makonda unafikiri suala lake lingefanyiwa kazi?
Matukio kama hayo yafanywayo na walioaminiwa na Serikali ndiyo yanayopeleka kufikiri kuwa huenda watumishi wa uma nchini ni miongoni mwa maadui wa nchi yetu.
Sijasema kuwa ni maadui, ila nimeuliza tu kuwa inawezekana watumishi wa umma ni adui wa nne wa nchi yetu? Kwamba, sasa nchi yetu ina maadui wanne: ujinga, magonjwa, umaskini, na watumishi wa umma?
Mkuu watumishi wa umma hawana tofauti na punda, nusu ya mishahara yao inarudishwa serikalini kama kodi, mfano (PAYE), wanakatwa na mifuko ya pension na hawapewi pesa yote waliyokatwa wakistaafu.
Kipindi cha Nyerere, maadui wa nchi walikuwa watatu: ujinga, magonjwa, na umaskini.
Ingawa hao maadui wangalipo, lakini huenda kuna adui mwingine kaongezeka: watumishi wa uma.
Mbaya zaidi ni kuwa huyo adui anaishi kwa jasho la wenye nchi kwa manufaa yake mwenyewe huku wenye nchi wakiumia.
Hapo chini ni clip ya mwananchi aliyezungushwa kwa miaka minne kupatiwa mchoro wa nyumba yake.
Fikiri, amelipa fedha zilizohitajika lakini bado alizungusha miaka yote hiyo. Kama asingekutana na Makonda unafikiri suala lake lingefanyiwa kazi?
Matukio kama hayo yafanywayo na walioaminiwa na Serikali ndiyo yanayopeleka kufikiri kuwa huenda watumishi wa uma nchini ni miongoni mwa maadui wa nchi yetu.
Sijasema kuwa ni maadui, ila nimeuliza tu kuwa inawezekana watumishi wa uma ni adui wa nne wa nchi yetu? Kwamba, sasa nchi yetu ina maadui wanne: ujinga, magonjwa, umaskini, na watumishi wa uma?
Hao wote wanasngukia kwenye kundi la watumishi wa uma:
1. Rais
2. Mawaziri
3. Wakuu wa mikoa
4. Wakurugenzi wa halmashauri n.k.
5. Maafisa ardhi
6. N.k.