Watumishi wa Umma sasa wameamka

Watumishi wa Umma sasa wameamka

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Tofauti na miaka mingine yote, kwa sasa watumishi wa Umma wameamka kutoka usingizini.

Wengi wao wameshagundua kuwa, mtetezi wao mkubwa si Wabunge wala serikali bali ni Viongozi wa vyama vya upinzani.

Hawa ndio watetezi wakuu wa watumishi wa Umma kwani husimama hadharani na kuyalalamikia mapunjo yao bila kupepesa macho tofauti na Wabunge waliopo sasa ambao hawana uthubutu hata kidogo kuwasemea watumishi wa Umma.

Nashukuru Mungu kwa kuwa sasa tunaanza kuelewana.
 
Hili wanalifahamu miaka yote, labda wewe ndiye ulikuwa hujui. Na ccm wanatambua hilo, ndio maana sasa unasikia bunge linasema watumishi wa umma wanalipwa kidogo, Walimu waongezewe mishahara.

Yote haya wanatengeneza mazingira ya kudanganya kwamba sasa wanayafanyia kazi matatizo ya watumishi wa umma.
 
Ni kweli, wanajifanya wanatetea maslahi ya watumishi wa Umma kumbe ni danganyatoto tu, ukishapita uchaguzi mambo ni yale yale
 
Hili wanalifahamu miaka yote, labda wewe ndiye ulikuwa hujui. Na ccm wanatambua hilo, ndio maana sasa unasikia bunge linasema watumishi wa umma wanalipwa kidogo, Walimu waongezewe mishahara. Yote haya wanatengeneza mazingira ya kudanganya kwamba sasa wanayafanyia kazi matatizo ya watumishi wa umma.
Mbunge selemani bungala "bwege" alisema mwishoooni mnaongeza mishahara, kesho nitaleta clip yake
 
Ikifika siku ya kampeni pilau na tembo(10,000) vinatosha kuwa sahaulisha yote hayo🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom